Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMC yasaka dawa mechi za ugenini

KMC Pict

Muktasari:

  • KMC ambayo ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo ikiwa na pointi 33 inatarajia kumaliza msimu kwa kucheza mechi mbili ugenini dhidi ya Mashujaa na kumaliza na Pamba Jiji.

KOCHA wa KMC, Adam Mbwana Mubesh, amesema kwa sasa yeye na kikosi hicho, wamejichimbia kutafuta dawa ya kusaka ushindi ugenini katika mechi mbili za kuamua hatma yao ya kucheza msimu ujao kwa kujenga umoja na ushirikiano baina na benchi na wachezaji.

KMC ambayo ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo ikiwa na pointi 33 inatarajia kumaliza msimu kwa kucheza mechi mbili ugenini dhidi ya Mashujaa na kumaliza na Pamba Jiji.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mubesh alisema anakumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi ugenini dhidi ya Tabora United Mei 14 mwaka huu akiifunga Tabora United bao 1-0 na ndio ulikuwa ushindi wake wa kwanza baada ya kukabidhiwa timu hiyo akianza na kichapo dhidi ya Simba.

“Haitakuwa rahisi lakini maandalizi yanaendelea pale tulipoishia na wachezaji wangu wapo kwenye hali nzuri ya ushindani tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya Mashujaa June 18 mchezo ambao utaamua nani anabaki nafasi aliyopo au nani anapanda kutokana na kufungana pointi,” alisema Mubesh na kuongeza;

“Tumebakiza siku chache kurejea kwenye kupambania nafasi ya kucheza msimu ujao, naamini vijana wangu wanatambua umuhimu wa mechi mbili zilizobaki kwa kuhakikishwa tunakusanya pointi zote tatu kikubwa ni kuheshimu wapinzani.”

Aliongeza, timu hiyo inahitaji umoja kushinda mechi mbili zilizosalia dhidi ya Mashujaa Juni 18 na Pamba Jiji Juni 22 huku akijivunia morali za wachezaji wake kuwa kwenye hali nzuri na anaamini watamaliza ligi kwa kishindwa kwa kukusanya pointi zote sita ugenini.

Kocha huyo alichukua mikoba ya Kally Ongala aliyeiongoza katika mechi 15 za Ligi Kuu Bara ambapo kati ya hizo, alishinda nne, sare nne na kupoteza saba.

Ongala aliyeifundisha pia Azam FC akiwa kocha wa mpito na kocha wa washambuliaji, alijiunga na KMC Novemba 14, 2024, akichukua nafasi ya Abdihamid Moallin aliyetimkia Yanga.

Awali, Mubesh aliwahi kufanya kazi Simba kabla ya kujiunga na KMC akiitumikia nafasi ya kocha wa viungo na utimamu wa mwili yaani (Fitness Coach), akiwa na taaluma ya ukocha inayompa fursa kubwa ya kukiongoza kikosi hicho cha Kinondoni.