Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMC yaiua Geita, Namungo yabanwa nyumbani

GEITA Gold ikiwa uwanja wa nyumbani imepoteza mchezo mbele ya KMC baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Nyankumbu, mjini Geita.

Hicho kilikuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Geita katika mechi za msimu huu, kwani mchezo uliopita ikiwa ugenini mjini Bukoba ilichapwa bao 1-0 kabla ya leo ikicheza kwa mara ya kwanza nyumbani msimu huu ilikumbana na kipigo hicho ambacho ni cha kwanza kwa timu nyumbani mbele ya KMC.

Katika mechi mbili za awali baina ya timu hiyo, Geita ilishinda moja na kulazimishwa sare moja, lakini jana bao la dakika tisa kutoka na Waziri Junior baada ya kipa Erick Johora kufanya uzembe alioporudishwa mpira na beki na mfungaji kumnyang'anya na kufunga, likiwa la pili kwa mshambuliaji kwa msimu huu.

Geita ilicharuka na kuchomoa bao hilo dakika ya 38 kupitia Tariq Seif.

Hata hivyo bao hilo lilidumu kwa dakika mbili tu, kwani KMC iliongeza nao la pili na lililokuwa la ushindi likiwekwa kimiani kwa kichwa na Juma Shemvuni akimalizia friikii ya Tepsie Evans kabla ya Geita kupata penalti dakika la majeruhi za kipindi cha kwanza, lakini nahodha wa timu hiyo, Elias Maguri aliipoteza.

Matokeo hayo yaliifanya KMC kupanda kutoka nafasi ya tisa hadi ya tano ikifikisha pointi saba baada ya mechi nne, huku Geita ikiporomoka kutoka nafasi ya sita hadi ya nane ikisaliwa na pointi nne.

Katika mechi nyingi iliyopigwa usiku kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi, wenyeji Namungo wametoka suluhu ya 0-0.