KMC yaipigia hesabu kali Ihefu

KLABU ya KMC kesho itaanza rasmi maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi Ihefu utakaochezwa Oktoba 7 katika uwanja wa Uhuru, Dar.
KMC imeingia leo asubuhi ikitokea Geita ilipokuwa na mechi dhidi ya Geita Gold mchezo uliochezwa Jumamosi iliyopita huku ikishinda 2-1.
Ofisa habari wa timu hiyo, Khalid Chukuchuku amesema wachezaji wote ambao walikuwa safarini wamepewa mapumziko na kesho watarudi.
"Leo timu itakuwa na mapumziko na kesho tutarudi kwa ajili ya maandalizi ya mechi yetu dhidi ya Ihefu itakayochezwa Jumamosi, hakuna majeruhi kwa wachezaji ambao walisafiri,"amesema Chukuchuku.
KMC katika mwezi Septemba imecheza mechi mbili na zote imeshinda, imeshinda 2-1 dhidi ya JKT Tanzania na 2-1 dhidi ya Geita Gold.
Timu hiyo itapata fursa ya kuwaangalia wapinzani wake hao watakapokuwa wanacheza na Yanga, Jumatano hii katika Uwanja wa Highlanda State, Mbarali.