Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiyombo kupigwa msasa kwanza

MAWAKALA wa straika Habibu Kiyombo wamepanga kumpeleka mchezaji huyo katika timu nyingine kwa mkopo ili kulinda kiwango chake kabla hajaanza kugombea namba ndani ya kikosi cha Mabingwa wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns iliyomsajili karibuni.

Kiyombo aliye chini ya kampuni ya Shadaka inayosimamia nyota mbalimbali wanafikiria kufanya hivyo kwa kile kilichoelezwa ni kuzoea soka la huko.

Mmoja wa mawakala wa kampuni hiyo, Ibrahim Mohamed aliliambia Mwanaspoti, mawazo yao watayawasilisha kwenye uongozi wa Mamelodi ambao watajadiliana kama watakubali kupelekwa kwa mkopo ama kubaki naye hapo.

Alisema lengo ni kupata muda wa kucheza kwani akibaki ndani ya kikosi hicho hatapata nafasi kirahisi ya kucheza kwa vile ligi ni tofauti.

“Bado yupo ndani ya Mamelodi hadi sasa, sisi ndio tunafikiria kumtafutia timu nchini humo itakayompa nafasi ya kucheza ili kuzoea soka la huko japo kwa miezi sita ndipo aingie kupambania namba Mamelodi.

“Mawazo yetu bado hatajawasilisha Mamelodi ila nadhani tutawasilisha na kuwasikiliza wao kama watakubali basi atakwenda kucheza kwa mkopo, wakigoma atabaki hapo.

“Kiyombo ametoka kwenye ligi tofauti na kule, hivyo kuingia moja kwa moja kikosi si rahisi sana na kwa kuona hivyo ndio maana tumefikiria kumtafutia timu kwa mkopo,” alisema Mohamed

Mamelodi iliyotwaa ubingwa msimu uliopita mbele ya Orlando Pirates ilimsajili Kiyombo kutoka Singida United aliyekuwa kinara wao wa mabao.