Kisa kadi, Carlinhos awaomba radhi Yanga

Sunday February 28 2021
yanga full pic 2
By Khatimu Naheka

Kiungo wa Yanga, Carlos Carmo 'Carlinhos'amelazimika kuiomba radhi klabu hiyo kufuatia tukio la kupewa kadi nyekundu.

Carlinhos amepata kadi hiyo dakika ya 79 wakati Yanga ikicheza dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa hatua ya mtoano wa Kombe la Shirikisho la Azam, kwenye Uwanja wa Uhuru.

CALOS MSAMAHA PIC

Kadi hiyo ilitokana na Carlinhos kuonyesha kuchukizwa na jinsi alivyodhibitiwa wakati akiwania mpira na beki wa kushoto wa Kengold Boniface Mwanjonde.

Wakati Mwanjonde akifanikiwa kumtuliza kiungo huyo raia wa Ureno wakiwa wanarejea uwanjani Carlinhos alionekana kushindwa kujizuia na kumpiga ngumi kwa nyuma beki huyo na baadaye kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 82.

Akiandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Carlinhos ameandika:" nawaomba radhi mashabiki timu, wachezaji wenzangu makocha na viongozi kwa kupata kadi nyekundu.

Advertisement

"Sasa nitainua kichwa changu juu baada ya adhabu hii kumalizika ili nirudi nikiwa imara ili timu iweze kufikia malengo yake ya msimu huu."

Hata hivyo baada ya kadi hiyo iliyowafanya Yanga kucheza takribani dakika 10 wakiwa pungufu Kengold haikuweza kubadili ubao wa matokeo na kumalizika Yanga wakishinda kwa bao 1-0 matokeo ambayo yamewafanya kusonga mbele.

Advertisement