Kipa Gor Mahia aingia gym na tahadhali ya corona

Muktasari:
Amesema hawezi kukaa bila kufanya mazoezi hivyo kila kinachotakiwa ajilinde nacho basi anabeba
Dar es Salaam. Kipa wa Gor Mahia, David Kisu amesema anapokwenda kufanya mazoezi ya gym anakuwa na vifaa vya kujilinda na maambukizi ya corona.
Amesema hawezi kukaa bila kufanya mazoezi hivyo kila kinachotakiwa ajilinde nacho basi anabeba.
"Najua ukigusa machuma ya gmy yanaweza kuhatarisha usalama wangu, sifanyi uzembe lazima niwe na sabuni na grovusi,"
"Siwezi kumwamini mtu yoyote katika hili kwa sababu nikifanya mchezo naweza kuhatarisha familia yangu na watu wanaonizunguka," amesema Kisu.
Ameshauri kila mchezaji lazima achukue tahadhari ya kulinda afya yake akiamini itasaidia kupunguza maambukizi.