Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinachoendelea kwa Chama, Yanga hiki hapa

Muktasari:

  • Mkataba wa Chama na Yanga utafikia tamati mara baada ya msimu huu kumalizika na pande hizo mbili zimeanza mazungumzo ya kuona kama kuna uwezekano wa kuwepo kwa mkataba mpya baina yao.

MASHABIKI wa Yanga kwa sasa wanasikilizia ishu ya Dabi ya Kariakoo kama itapigwa au la, lakini kuna kitu kinaendelea ndani ya klabu hiyo kuhusu kiungo mshambuliaji, Clatous Chama.

Mkataba wa Chama na Yanga utafikia tamati mara baada ya msimu huu kumalizika na pande hizo mbili zimeanza mazungumzo ya kuona kama kuna uwezekano wa kuwepo kwa mkataba mpya baina yao.

Hata hivyo, katika mazungumzo hayo kila upande umeonekana kutoa sharti ambalo linaonekana kuwa gumu kwa mwingine na kama wasipofikia muafaka, kiungo huyo Zambia anaweza kufunguliwa mlango wa kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Chanzo cha uhakika ndani ya Yanga kimelifichulia Mwanaspoti kuwa, timu hiyo imempa sharti moja Chama ambalo ni kumpa dau pungufu la usajili tofauti na lile ambalo ilimpatia ilipomnasa mwaka jana baada ya nyota huyo kumaliza mkataba wake na Simba. Chama alisaini mkataba wa mwaka mmoja msimu uliopita ambapo alivuta kiasi kinachokadiriwa kufikia Dola 150,000.

Katika mazungumzo ambayo wameanza, Chama ameweka sharti la kupewa dau kama hilo au zaidi ili asaini mkataba jambo ambalo uongozi wa Yanga hauko tayari kulifanya na badala yake utakuwa tayari kumpa fedha pungufu ya hizo ilizotoa mwaka jana.

“Kila upande unashikilia msimamo wake. Uongozi unataka kumpa mkataba mpya kwa dau la chini la fedha kulinganisha na lile alilopata mwaka jana alipojiunga na mchezaji mwenyewe anataka zaidi au ikishindikana basi apewe angalau kiasi kama alichopata aliposaini mkataba unaomalizika,” kilisema chanzo hicho.

“Tumempa muda wa kutafakari na kama atashikilia msimamo wake tutaachana naye kwa vile hatuwezi kutoa fedha nyingi kwa mchezaji ambaye umri umesogea na kiwango chake sio kile cha nyuma.”

Katika msimu huu, Chama amekuwa sio miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Yanga na amekuwa hapati muda mwingi wa kucheza hivyo haendani na thamani ya fedha anaihitaji.

Mchezaji huyo ana wastani wa kucheza kwa dakika 37.4 kwa mchezo katika Ligi Kuu kwani ametumika kwa dakika 748 tu katika michezo 20 ya Ligi Kuu.

Hata hivyo, pamoja na kutokuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza, Chama ameonyesha ana akitu kwani amehusika na mabao sita ya Yanga, akifunga manne na kuasisti mbili, lakini akiwa amefunga mawili katika Kombe la Shirikisho (FA), Yanga ikiwa imetinga fainali ikisubiri kucheza na Singida BS. Katika eneo la kiungo mshambuliaji, benchi la ufundi la Yanga msimu huu limekuwa likiwatumia zaidi Stephane Aziz Ki ambaye tayari ameshaachana na timu hiyo na kujiunga na Wydad ya Morocco na Pacome Zouzoua ambaye bado yupo katika kikosi cha Yanga sambamba na Mudathir Yahya.