Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilanga aibuka mbabe, amtwanga Mwakisu

Hashim Kilanga (wa pili kutoka kulia) akipunga mkono baada ya kutangazwa bingwa kwa kumtwanga mpinzani wake, Donard Mwakisu (wa pili kutoka kushoto)

Mbeya. Baada ya tambo za muda mrefu, hatimaye Mbeya ilimpata mbabe wa masumbwi, Hashim Kilanga aliyemmaliza mpinzani wake, Donald Mwakisu kwa pointi katika pambano la raundi nane.

Kwa muda mrefu wawili hao walikuwa wakitambiana kwa kila mmoja akidai ni mbabe katika mchezo wa ngumi, ambapo ubishi uliisha usiku wa kuamkia leo walipopanda ulingoni kuzipiga kavukavu.

Katika pambano hilo, pamoja na kila upande kuonesha uimara lakini Kilanga alionekana kuwa mjanja haswa kwenye kusaka pointi dhidi ya mpinzani wake kutokana na ngumi zake kufika eneo stahiki.

Mashabiki waliokuwa wakishangilia mwanzo mwisho upande wa Mwakisu walibaki wameinamisha vichwa chini baada ya kutangazwa kwa matokeo ya jumla na kuamsha shangwe kwa upande wa Kilanga.

Pambano hilo ambalo lilifanyika wilayani Chunya, lilikuwa la kwanza kuwakutanisha wababe hao kutoka Wilaya tofari za Mkoa huo, ikiwa ni Mbalizi na Uyole likilenga kumpata bingwa wa Mkoa.

Hata hivyo kabla ya pambano hilo la usiku, zikitanguliwa ngumi za ufunguzi, ambapo Sam Mputi alimchakaza kwa TKO raundi ya tano Joseph Kabolile, huku Ambokile Chusya akifa pia kwa TKO raundi ya kwanza kati ya sita dhidi ya Aruto Kienga ilhali Joseph Sinkala akishinda kwa pointi mbele ya Six Bruno.

Akizungumza baada ya mapambano hayo, mwenyekiti wa Chama cha ngumi za kulipiwa Mkoa wa Mbeya,(PBC) ambaye ndiye aliandaa shindano hilo, Gardner Mwakasyuka amesema lengo ni kupata bingwa wa Mkoa, lakini kuibua vipaji kwa vijana na kuwapa nafasi kuonesha uwezo wao.

"Niombe wadau inapotokea shughuli kama hii yenye maslahi kwa vijana na mkoa wetu basi kuwepo na muitikio wa kusapoti, muda mwingine na sisi wadau tunavunjika moyo tunapoandaa mashindano haya tukakosa nguvu" amesema Mwakasyuka ambaye ni Promota.