Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikoti yeye na Coastal Union

KIKOTI Pict

Muktasari:

  • Kikoti amesema anathamini kipindi alichokaa ndani ya kikosi cha Wagosi wa Kaya, haoni sababu ya kuwahi kufanya uamuzi wa kujiunga na timu nyingine kabla hajatoa nafasi kwa Coastal kujipanga.

KIUNGO Lucas Kikoti ameweka wazi kuwa, licha ya mkataba wake kumalizika rasmi mwishoni mwa msimu huu, moyo wake bado uko Coastal Union na hiyo ndiyo sababu anataka kuipa kipaumbele klabu hiyo kabla hajafanya uamuzi mwingine kuhusu mustakabali wake.

Kikoti amesema anathamini kipindi alichokaa ndani ya kikosi cha Wagosi wa Kaya, haoni sababu ya kuwahi kufanya uamuzi wa kujiunga na timu nyingine kabla hajatoa nafasi kwa Coastal kujipanga.

Kwa mujibu wa nyota huyo, uamuzi wake unaongozwa na heshima aliyonayo kwa uongozi, mashabiki na mazingira ya timu hiyo yenye maskani yake jijini Tanga.

“Nimekuwa hapa kwa miaka miwili na huu si muda mchache. Ni muda wa kujenga misingi ya uaminifu na mshikamano. Nimetimiza mkataba wangu lakini naamini si vibaya kuisubiri Coastal kwanza. Ni timu ambayo imenipa nafasi, na ni muhimu kuonesha shukrani kwa namna hiyo,” alisema Kikoti.

Nyota huyo ambaye alijiunga na Coastal Union Julai 2023 akitokea Namungo, kwenye mechi ya mwisho ya msimu, alifunga bao lililoisaidia timu hiyo kupata sare ya 1-1 dhidi ya Tabora United katika Dimba la Mkwakwani, Tanga.

Sare hiyo iliwasaidia Coastal Union kumaliza msimu katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. 

Wakati baadhi ya klabu zikianza kuonesha nia ya kumsajili, Kikoti alisema hana pupa. Anachotaka ni kusikia mustakabali wake kutoka kwa viongozi wa Coastal.

Alisisitiza kama mazungumzo yataenda vizuri, yuko tayari kusaini mkataba mpya na kuendelea kuitumikia timu hiyo.