Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikosi cha Feisal, Yanga 5 Simba 2

FEISAL Pict

Muktasari:

  • Fei ambaye aliwahi kuichezea Yanga misimu miwili iliyopita amekuwa miongoni mwa mastaa wazawa wenye uwezo mkubwa ambao wamewahi kuwatoa jasho wachezaji wa kigeni, ambapo kwa sasa anamiliki mabao manne na asisti 13 akiwa ndiye kinara wa pasi za mwisho katika Ligi Kuu Bara.

LIGI Kuu Bara imesaliwa na jumla ya mechi 17 kabla ya msimu kufikia tamati, lakini kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amevunja ukimya kwa kutangaza kikosi chake cha msimu akiwajumuisha nyota watano wa Yanga na wawili wa Simba.

Fei ambaye aliwahi kuichezea Yanga misimu miwili iliyopita amekuwa miongoni mwa mastaa wazawa wenye uwezo mkubwa ambao wamewahi kuwatoa jasho wachezaji wa kigeni, ambapo kwa sasa anamiliki mabao manne na asisti 13 akiwa ndiye kinara wa pasi za mwisho katika Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti alisema msimu huu umekuwa na mastaa wengi wenye viwango vikubwa, lakini wapo ambao wameukosha moyo wake ambapo amewataja katika kikosi cha msimu hata kabla ligi haijamalizika.

“Nitawataja mastaa wangu bora zaidi wa msimu huu kwa upande wangu na nimechanganya wageni na wazawa katika timu tofauti ingawa naichezea Azam, ila wapo wa Yanga na Simba pia,” alisema Fei aliyemaliza kama mfungaji namba mbili msimu uliopita akifunga mabao 19 na asisti saba nyuma ya aliyeibuka kinara Stephane Aziz KI aliyekuwa Yanga aliyefunga mabao 21 na asisti nane.

Fei alisema kikosi hicho ni mtazamo wake kwa msimu huu na watu wasimchukulie sivyo, kwani Ligi Kuu Bara ina mastaa kibao na kila mtu ana chaguo lake.

Staa huyo aliwataja mastaa wake bora wa kikosi cha kwanza na kusema kwa upande wa kipa lngoni anakaa Diarra Djigui, huku beki wa kuli ni Lusajo Mwaikenda na kushoto akiwa ni Pascal Msindo, Ibrahim Bacca, Yesion Fuentes, Yusuf Kagoma/Duke Abuya, Pacome Zouzoua, Prince Dube, Feisal Salum na Jean Charles Ahoua.

Nyota huyo wa Kizanzibari amerejea kutoka katika majukumu yake ya timu ya Taifa, huku akiwa hajacheza baadhi ya mechi kutokana na majeraha aliyoyapata ilhali timu ya Azam ikisaliwa na mechi mbili za kufungia msimu wakati ikiwa katika nafasi ya tatu ikimiliki pointi 57.