Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiiza atonesha kidonda Simba

Kiiza aamua kuvunja ukimya

NAHODHA msaidizi  wa Kagera Sugar Mganda Hamisi kiiza amesema hana hofu na Simba na anatarajia  kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wao wa kesho utakaopigwa katika uwanja wa Benjamini mkapa Dar es Salaam saa 1:00 usiku.

Simba kuelekea mchezo wa kesho wana kumbukumbu mbaya na mshambuliaji huyo aliyeisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wa kaitaba Januari 26 mchezo wa kwanza baina ya timu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nahodha huyo amesema yeye kama kiongozi wa wachezaji anashikiria malengo ya kupata ushindi licha ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya  Azam kwa kufungwa mabao 2-1.

“Mchezo wa kesho na simba ni mchezo mwepesi kwangu  kwani ukijipanga kupata matokeo mazuri ndio unayatapa lakini ukiwa na hofu utayakosa hivyo sisi kama wachezaji tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata ushindi,” amesema Kiiza aliyewahi kucheza Simba na Yanga.

Aidha nyota huyo mkongwe ameweka wazi kuwa kocha mchezaji ndani ya kikosi hicho kwani amekuwa akiwafundisha na kuwaelekeza ndani na nje ya uwanja.

“Mara nyingi naongea na wachezaji wenzangu na kuwasisitiza kujitoa katika uwanja ili tuweze kutimiza malengo yetu binafsi na ya timu unapoingia uwanjani kwa malengo ndio unapata unachokihitaji.”

Msimu uliopita katika mechi ya kwanza ya ligi, Kagera ikiwa nyumbani iliifunga Simba 1-0 bao likifungwa na Kiiza na katika mechi ya marudiano iliyopigwa uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda 2-0.