Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibuta kuanza na Geita, muda wapanguliwa

Muktasari:

  • Wachezaji hao kutokea Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, wanasubiri kuitumikia timu hiyo pamoja na ligi kuu bara kwa mara ya kwanza.

MCHEZAJI Mwana Kibuta, hatimaye anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza katika timu ya Dodoma Jiji dhidi ya Geita Gold kesho Alhamisi, baada ya kupata kibali cha kazi, kiongozi wa juu wa timu hiyo amethibitisha.


Kiungo huyo kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pamoja na mwenzake Randy Bangala ndio wachezaji pekee ambao walikua bado hawajapata vibali vya kuwawezesha kucheza mechi za timu hiyo, tangu waliposajiliwa.


Randy ambaye ni mdogo wa Yannick Bangala wa Yanga, atalazimika kusubiri hadi mchezo ujao dhidi ya Simba ili kujua hatma ya kucheza endapo kibali chake kitakamilika, ila kwa Kibuta ni rasmi ameshapata na mchezo wa Geita kesho atacheza.


Mchezo baina ya Dodoma Jiji na Geita umelazimika kubadilishwa muda mara mbili, awali ulikuwa uchezwe majira ya saa 1 jioni katika uwanja wa Jamhuri, ukabadilishwa uwanja kuwa Liti muda wa saa 10 jioni na sasa umewekwa saa nane mchana.


Kutofunguliwa kwa uwanja wa Jamhuri ambao una siku 10 tangu ukaguliwe, lakini imeshindikana kufunguliwa na kufanya timu ya Dodoma Jiji kubaki kuchezea Liti Singida, kumalizia mchezo huo dhidi ya Geita.


Timu zote mbili hazijashinda mchezo katika ligi, Geita wakiwa na sare tatu wakipoteza mchezo mmoja, Dodoma Jiji wakiwa na sare mbili na kupoteza mechi mbili.