Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kasi ya kriketi yaipa kicheko TCA

KRIKET Pict

Muktasari:

  • Kasi hiyo ya kukuza vipaji imeonekana katika baadhi ya mikoa ya Pwani, Nyanda za Juu Kusini, Nyanda za Juu kaskazini, Kanda ya Kati na Kanda ya Ziwa kuanza kuzaa matunda na kuondoa ufalme wa Dar es Salaam.

CHAMA cha Kriketi Tanzania (TCA) kinaiona kesho ya ngavu katika mchezo huo kutokana na kasi ya ukuaji katika mikoa mingi ya Tanzania.

Kasi hiyo ya kukuza vipaji imeonekana katika baadhi ya mikoa ya Pwani, Nyanda za Juu Kusini, Nyanda za Juu kaskazini, Kanda ya Kati na Kanda ya Ziwa kuanza kuzaa matunda na kuondoa ufalme wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa TCA, Dk Balakrishna Sreekumar alisema; “Chama cha Kriketi Duniani (ICC) kimeguswa sana na namna kriketi inavyoshamiri nchi nzima kwa kuwashirikisha vijana wengi wa shule za msingi, sekondari na vyuo katika zoezi linakwenda sambamba na uandaaji wa wakufunzi wa mchezo huu katika shule hizo.

Alisema chama chake kinakishukuru ICC kwa misaada yake katika kuiwezesha Tanzania kuyafikia mafanikio haya na zoezi la kusaka vipaji na kuviendeleza linakwenda sanjari na utenegezaji wa viwanja vipya vya mchezo huu.

Alisema kukamilika kwa uwanja wa kisasa wa UDSM na vingine katika maeneo ya Chanika, Kigamboni, Gairo, Mwanza, Iringa na Arusha, kutasaidia kuzalisha vipaji zaidi na Tanzania itaanza kutengeneza wachezaji wengine wa kulipwa kama ilivyokuwa kwa Khalil Rehmtullah, Benson Mwita, Hamis Abdallah na Athumani Kakonzi ambao miaka kadhaa iliyopita walikuwa Watanzania wa kwanza kucheza kriketi ya kulipwa England.

TCA pia inaona nyota njema kwa wachezaji wengi wa timu ya taifa ya vijana wa chini ya miaka19 kwa kuwa wana nafasi kubwa ya kuwa wachezaji wa kulipwa baada ya kushiriki fainali za kombe la dunia kwa vijana wa chini ya miaka 19.