Kaseja mabosi wake wamemuelewa

Muktasari:
- Kaseja ambaye alianza kazi mwanzoni mwa mwezi machi,Baada ya kuondoka kwa kocha Melis Medo aliyetimkia zake Singida Black Stars.
UONGOZI wa Kagera Sugar ya kocha Juma Kaseja, umesisitiza kwamba una imani na staa huyo aliyepewa timu hivikaribuni na tena walichelewa kumpa kazi hiyo.
Kaseja ambaye alianza kazi mwanzoni mwa mwezi machi,Baada ya kuondoka kwa kocha Melis Medo aliyetimkia zake Singida Black Stars.
Kabla ya uwepo wa kocha huyo,Kagera ilikuwa na rekodi ya kucheza mechi 22, ikishinda mityatu,sare sita, kupoteza 13.
Hii ni kwa mara ya kwanza kwa Kaseja kuwa kocha Mkuu kwani hapo awali alikuwa mwalimu wa makipa, huku akiibua timu hiyo kutoka nafasi ya 15 iliyoachwa na mwalimu aliyepita mpaka ya 14, ikiwa na pointi 16.
Staa huyo wa zamani wa Simba,Yanga,tangu akabidhiwe kijiti hicho amecheza mechi tatu za Ligi Kuu na kushinda mbili.
Alianza na Pamba Jiji ambao aliichapa 2-1 na Coastal Union kuwapa kichapo hicho bila huruma.
Huku mechi ya tatu juzi ikiwa ugenini ilijikuta inapoteza mchezo wake wa kwanza chini yake ilipofungwa na Tanzania Prisons kwa bao 1-0, lililofungwa na nahodha wa wanajeshi hao Haruna Chanongo.
Kupitia Mwanaspoti Kaseja aliwahi kusema kuwa;"Nawapongeza wachezaji wangu kwa kucheza kwa kupambana na bidii kubwa ili kuhakikisha Kagera inasalia katika ligi msimu ujao.
"Nimefanya kazi na Kagera kama kocha wa makipa na uongozi ulinipa heshima hii kubwa, lakini kuna baadhi ya wachezaji tunafahamiana na niliwahi kucheza nao, hivyo tunapokuwa na mechi tunakaa na kukubaliana nini tufanye."
Akizungumza na Mwanaspoti Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kagera Ramadhan Kalula alisema sio tu kikosi chao bali kampuni nzima ya Kagera ina imani kubwa na Kaseja ambaye ndani ya mechi nne za kwanza hakupoteza mchezo wowote.
Kalula alisema Kagera chini ya Kaseja kuna muamko mkubwa kwa wachezaji wake,wakionyesha kurudisha hali ya kuipigania timu ambapo ni kama walichelewa kumrudisha kocha huyo.
"Tuna imani kubwa na Kaseja, sisi tulio ndani ya timu tunaona mabadiliko makubwa kuanzia morali ya wachezaji wetu wamekuwa na juhudi kubwa sana lakini hata namna timu inavyocheza unaona mambo yamebadilika sana,"alisema Kalula.
"Kaseja hapa Kagera ni nyumbani alikuwa hapa kama mchezaji, baadaye akapewa jukumu la kufundisha akaondoka na kurudi tena, sisi viongozi tunaona kama tulichelewa kumrudisha, tunaimani kwamba tutabaki ligi kuu.
Kagera ambayo imeanza kuona nyote njema,inashika nafasi ya 14 katika msimamo,ikiwa imebakiza mechi tano mkononi kati ya 30 ili kumaliza msimu huu, ikifikisha jumla ya pointi 22.