Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jeshi la Polisi latoa uhakika wa usalama Kariakoo Dabi

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limewahakikishia usalama wananchi katika mechi ya Simba na Yanga inayotarajiwa kuchezwa kesho Jumatano Juni 25, 2025 huku ikiwaonya wenye lengo la kuleta vurugu na udhalilishaji.

Mchezo huo namba 184 wa raundi ya pili wa Ligi Kuu ambao awali ulipangwa kuchezwa Machi 8, 2025, uliahirishwa baada ya Simba kudai kuzuiwa na wanaodaiwa kuwa walinzi wa Yanga kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa siku moja kabla ya mechi ikiwa timu mgeni.

Tukio hilo lilizua mtafaruku mkubwa kuelekea mchezo huo ambapo Bodi ya Ligi Kuu ilitangaza kuhairishwa kwa mchezo, huku Yanga wakitoa tamko kuwa hawatacheza tena mechi hiyo.

Hivi karibuni TPLB ilitangaza rasmi mechi hiyo ya dabi itapigwa Juni 15, 2025. Hata hivyo Yanga waliibuka tena na kuzidi kutilia mkazo msimamo wao wa kutoshiriki mchezo huo, huku Simba wakiwa wametangaza kuingia kambini.

Akizungumza leo Jumanne Juni 24,2025 na waandishi wa habari  kuhusu mtanange huo,  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Jeshi hilo  linatambua kuwa kesho (Juni 25,2025) majira ya saa 11 za jioni kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa Temeke kutakuwa na mchezo wa soka wa timu mbili ambazo ni watani wa jadi Simba na Yanga zote za jijini Dar es Salaam.

"Jeshi linatambua kwamba mchezo huu utakusanya watu wengi wa kutoka ndani na nje ya Dar es Salaam.

"Kutokana na mkusanyiko mkubwa wa wapenzi wa soka wanaotarajiwa kufika katika uwanja huo, amesema Jeshi hilo limejipanga vizuri kuhakikisha kwamba suala la usalama katika uwanja huo linakuwa la hali ya juu kabla, wakati na baada ya mchezo huo,"amesema Kamanda Muliro.