Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kakway anacheka tu na nyavu huko

Muktasari:

  • Wachezaji wengine wanaomfuatia na timu zao katika mabano ni Jonas Mushi (JKT) 44, Emanuel Kibona (KIUT) 42,Sam Aguti (Mchenga Star) 38, Baraka Sadiki (JKT) 37. Wengine ni Isaya Wiliam (DB Oratory) 36, Ferix Luhamba  (JKT) 35, Oscar Mwituka (Savio) 35, Jamel Marbuary (Dar City) 34 na Charles Allson (Crows) 34.

WAKATI mafundi wa kutupia katika maeneo ya mitupio mitatu ‘three pointi’ wakichuana vikali katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa dar es Salaam (BDL), mchezaji Abdul Kakwaya wa DB Oratory anaongoza kufunga ‘three pointi’ 55.

Wachezaji wengine wanaomfuatia na timu zao katika mabano ni Jonas Mushi (JKT) 44, Emanuel Kibona (KIUT) 42,Sam Aguti (Mchenga Star) 38, Baraka Sadiki (JKT) 37. Wengine ni Isaya Wiliam (DB Oratory) 36, Ferix Luhamba  (JKT) 35, Oscar Mwituka (Savio) 35, Jamel Marbuary (Dar City) 34 na Charles Allson (Crows) 34.

Naye chipukizi wa Vijana,   Stanley Mtunguja (18) anayechezea timu ya Ukonga Kings anazidi kuwaacha kwa mbali wakongwe wa mchezo huo baada ya kuongoza kwa kutoa asisti mara 108.

Nyota huyo anafuatiwa na   Cornelius Mgaza wa Savio aliyetoa asisti 81, Amin Mkosa (Mchenga Star) 81, Alinani Msongole (ABC) 77 na Evance Davies (Outsiders) 77

Wengine ni  Ally Abdalah (Dar City ) 67  Dominic Kipingu (DB Oratory) 67, Joas Maheta (Savio) 64, Josephat Petar  (DB Oratory) 62 na Alex Bwana (Mchenga Star) 60.