Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kakolanya: Makundi yanatuhusu CAF

Muktasari:

  • Timu hizo zitakutana Oktoba Mosi katika Uwanja wa Al-Salaam, Cairo, Misri, huku Singida ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata wiki iliyopita Dar.

KIPA wa Singida Fountain Gate, Beno Kakolanya amesema licha ya mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Future ya Misri utapigwa ugenini, lakini anaiona nafasi ya timu yao kutinga makundi ya michuano hiyo.

Timu hizo zitakutana Oktoba Mosi katika Uwanja wa Al-Salaam, Cairo, Misri, huku Singida ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata wiki iliyopita Dar.

Akizungumzia mchezo wa ugenini, Kakolanya alisema Simba na Yanga zimejiweka pazuri kutinga makundi Ligi ya Mabingwa, lakini wao ni ngumu kwa kuwa walianzia nyumbani na ushindi mwembamba.

Hata hivyo, kipa huyo wa zamani wa Yanga na Simba alisema ushindi waliopata nyumbani unawapa nguvu  ya kutinga makundi na kwamba kila mchezaji atajitolea kuhakikisha anapata matokeo mazuri.