Kahama Sixers yaendeleza moto

Muktasari:
- Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana fainali ya mwaka jana, Kahama iliishinda Risasi michezo 3-1.
KLABU ya Kikapu ya Kahama Sixers imeanza vizuri kampeni ya kutetea taji la ubingwa wa Ligi ya Mkoa wa Shinyanga, baada ya kuifunga Risasi kwa pointi 54-46, katika mchezo uliopigwa kwenye Uuwanja wa Kahama, mjini humo.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana fainali ya mwaka jana, Kahama iliishinda Risasi michezo 3-1.
Kahama Sixers ilianza mchezo kwa robo ya kwanza kwa kasi, hali iliyofanya iongoze kwa pointi 19-11, robo ya pili, Risasi iliongoza kwa pointi 16-8.
Robo ya tatu ilipoanza mchezo ulizidi kuwa mkali na kila timu kuongeza kasi na kuwa mchezo wa funga nikufunge, hadi robo hiyo inamalizika zilikuwa zimefungana pointi 11-11 na robo ya nne Kahama ikapata pointi 16-8.
Kwa ufungaji, Vicent Mangula wa Risasi, alitupia pointi 16 akifuatiwa na Hemed Magoti aliyefunga 13.
B4 Mwadui, Risasi, Kahama Sixers na Veta ndizo zinazoshiriki na Kamishina wa Ufundi na Mashindano wa Ligi ya Kikapu Shinyanga, George Simba, alisema mfumo wa ligi hiyo, kila timu itacheza nyumbani na ugenini ili kuja kupata bingwa wa msimu huu.