Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagere, Kibu kuiongoza Simba

KOCHA wa Simba, Pablo Franco amemuanzisha mshambuliaji wake Meddie Kagere katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya RS Berkane katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Nyota huyo anachukua nafasi ya John Bocco ambaye anakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja aliyoyapata kwenye mchezo wa mwisho wa ligi na Dodoma Jiji.

Mabadiliko mengine ambayo Pablo ameyafanya ni kwenye idara mlinda mlango ambapo Aishi Manula amerudi baada ya kukosa mechi mbili za ligi kutokana na kusumbuliwa na matatizo wa kifamilia.

Naye winga Kibu Denis aliyekuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha amerudishwa kikosini kuwakabili RS Berkane.

Kikosi kamili cha Simba ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Henock Inonga, Joash Onyango, Jonas Mkude, Sadio Kanoute, Pape Sakho, Larry Bwalya, Meddie Kagere na Denis Kibu.

Wachezaji wa akiba ni Beno Kakolanya, Israel Mwenda,  Keneddy Juma, Bernard Morrison, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin, Peter Banda na Chriss Mugalu.


MASHABIKI KIBAO KWA MKAPA

Simba wanajambo lao leo hivyo ndio unaweza ukasema kutokana na mashabiki wa timu hiyo walivyojitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao.

Simba ambao ndio wawakilishi pekee kwenye mashindano ya kimataifa, wanashuka dimbani kumenyana na RS Barkane kwenye mchezo wa makundi D Kombe la Shirikisho Afrika.

Mastaa wa Simba wanashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 2-0 ugenini na kujikuta wanaporomoshwa kutoka nafasi ya kwanza hadi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo