Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagere fresh, bado Kazadi

BAADA ya Meddie Kagere hatimaye kufuta gundu la kutofunga muda mrefu, shughuli pevu imebaki kwa Francy Kazadi.

Kagere alifunga bao lake la kwanza msimu huu, akiunganisha vema mpira wa friikiki iliyopigwa na Bruno Gomes kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union.

Bao hilo ni kama limefungua njia kwake Kagere kusaka mabao zaidi ambapo pia amekuwa akipatiwa nafasi ya kuanza zaidi tangu ujio wa kocha mpya tofauti na makocha waliotangulia.

Hata hivyo, hali bado ni ngumu kwa straika Francy Kazadi ambaye anakaribia mwaka bila kufunga bao tangu alipofanya hivyo kwenye michuano ya Mapinduzi ya Januari mwaka huu.

Kazadi bado hajafunga bao kwenye mechi za Ligi Kuu Bara tangu asajiliwe kwenye dirisha dogo lililopita.