Kagere, Fraga kuikosa Yanga SC Jumamosi

Muktasari:
Simba inatarajia kukutana na Yanga katika mchezo wao wa kwanza wa mahasimu katika Ligi Kuu msimu huu Uwanja wa Mkapa.
Dar es Salaam. Kinara wa mabao katika kikosi cha Simba, Meddie Kagere aliyefunga manne na kiungo raia wa Mbrazil, Person Fraga rasmi hawatakuwa katika kikosi kitakachoivaa Yanga Jumamosi.
Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck ameliambia gazeti hili jana kuwa majeraha ambayo aliyapata Kagere katika mechi na JKT Tanzania yatamuweka nje si chini ya wiki mbili hadi tatu.
Sven alisema kukosekana kwa Kagere si habari njema kwao haswa wanapokutana na mechi ngumu dhidi ya timu ambayo wapo nayo kwenye mbio za kiwanja ubingwa, ila kukosekana kwake atatoa nafasi kwa mchezaji mwengine.
“Habari mbaya zaidi ndani ya timu ni kumkosa Fraga, ambaye atakuwa nje ya uwanjani wa kipindi kisichopungua miezi sita, kwahiyo naye hatakuwa katika kikosi ambacho kitacheza na Yanga,” alisema Sven.
“Lakini hata mshambuliaji mwingine, Chris Mugalu, bado hatujafahamu majibu ya tatizo lake kama ataweza kuwepo katika mechi na Yanga au atakosekana kama ilivyokuwa kwa Kagere na Fraga.
“Tutawakosa wachezaji hao, lakini kiu yetu kubwa ni kupata pointi tatu dhidi ya Yanga ili kupunguza umbali wa pointi sita ambazo walituacha kutokana kuwa na wiki mbaya ya kupoteza mechi mbili,” alisema Sven.
Katika hatua nyingine, daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema majeraha ambayo aliyapata Kagere na Fraga, ambaye aliumia goti ni wachezaji wachache mno ambao hupona kwa haraka.
Gembe alisema Kagere anaweza kurejea haraka kutokana na jeraha lake la mguu kuendelea vizuri, lakini Fraga inabidi apate matibabu zaidi ya goti na baada ya hapo apate muda wa kutosha kupumzika.
“Wote wawili kama ilivyoeleza kocha ni ngumu kuwepo katika mechi na Yanga ila kubwa ambalo linafanyika wakati huu ni kupewa uangalizi na matibabu ya kila wakati ili ndani ya muda sahihi waweze kupona na kurejea katika majukumu yao,” alisema Gembe.
Simba walikutana na Yanga mara ya mwisho kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC), Fraga alianza katika kikosi cha kwanza na alifunga bao la kwanza wakati Kagere aliingia kwenye kipindi cha pili na kupiga shuti kali ambalo, Metacha Mnata alilipangua na Mzamiru Yassin kuifungia timu yake bao la nne.
Kagere tangu amekuja nchini kucheza soka amekutana na Yanga katika mechi tano na amewafunga mabao mawili yote yakiwa kwenye ligi moja la kichwa na lingine penalti.
Sven apigwa presha
Katika hatua nyingine, Sven alisema alikuwa na wiki mbaya ambayo alikutana na presha kutoka katika maeneo mbalimbali baada ya timu yaje kufungwa mechi mbili mfululizo za ligi.
Sven alisema alikutana na presha pamoja na maneno mengi kutoka kwa mashabiki na watu wengine aliyapokea kukubaliana nayo kwa kuwa alifahamu ukifundisha timu kubwa lazima utakutana na jambo kama hilo.
“Tuliingia na malengo makubwa ya Kutoka ushindi katika mechi ya Mwadui kuliko jambo lolote, ndiyo maana ukiangalia hata tulivyocheza tulikuwa na mlengo huo, huku tukiwa na nidhamu kubwa katika kuzuia ili yasitokee yale yaliyotukuta katika mechi mbili zilizopita,” alisema.
“Tumetengeneza nafasi nyingi za kufunga na tumetumia tano, kubwa ambao tulitaka ni ushindi ili kurudisha imani kwa mashabiki na wachezaji kujiamini na baada ya hapo ndiyo tutaanza kuangalia mambo mengine na tutayafanya katika mechi ijayo na Kagera Sugar.
“Nawapongeza wachezaji wangu wamekwenda kufanya kile ambacho nilikuwa nahitaji kutoka kwao haswa mbele ya timu ambayo ilikuwa ni nidhamu kubwa ya kucheza kwa kuzuia,” alisema Sven.
Kusitishwa kwa huduma hiyo kumesababisha mrundikano wa maombi ya hat mara ya kwanza na wale wanaotaka mpya baada ya za awali kujaa au kumalizika muda wake.