Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kadi za Yanga zazua balaa Arusha

Ikiwa zimebaki Dakika chache kabla mchezo wa Yaga dhidi ya Polisi Tanzania kuanza, huko nje baadhi ya mashabiki wameshindwa kuingia kuutazama mchezo huo mubashara kutokana na kadi zao kukataliwa kwenye mtandao (system)

ARUSHA. Ikiwa zimebaki Dakika chache kabla mchezo wa  Yaga dhidi ya Polisi Tanzania kuanza, huko nje baadhi ya mashabiki wameshindwa kuingia kuutazama mchezo huo mubashara kutokana na kadi zao kukataliwa kwenye mtandao (system)

Mchezo huo wa 103 mzunguko wa 13 wa Ligi Kuu ya NBC, unatarajiwa kuanza Majira ya saa kumi jioni, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Katika Hali isiyo ya kawaida, kadi walizokuwa wanakata mashabiki  wa Yanga kwa ajili ya kuwa  mwanachama  zitakazokuwa zinatumika pia kulipia viingilio na Ada (N-kadi), zimekuwa mwiba kwao leo baada ya kulipia lakini bado mtandao ukawakataa.

"Mimi nimetoka Moshi nimelipia kadi yangu pale kwenye gari, VIP B shilingi 10,000 kwa kadi yangu hii hapa lakini nashangaa nimefika hapa getini wanaingiza wanasema imesatumika,.. Sasa imetumika vipi wakati mechi ni leo  ndio naingia??" Alisema Aisha  Shabani aliyetolewa kwenye foleni.

Nae Charles John alisema kuwa amekuja na kadi yake na kulipia lakini anasema imekataliwa kwa madai haitambuliki.

"Kadi nilinunua Dar hii na nimelipia kuja kutazama hii mechi nashangaa naambiwa kadi haitambuliki wakati hela imemezwa, hapa nasubiri utaratibu  ni upi maana nasukumwa tu hapa sielewi na hakuna anaenisikiliza" alisema Charles

Wenye kadi yao, Hassan Bumbuli afisa habari wa Yanga, amesema kuwa kwa Sasa hawezi kuzungumzia swala hilo kwani mechi ni ya Polisi lakini watafuatilia malalamiko hayo.

"Hii mechi sio yetu, Sasa ikiniuliza maswala ya kadi au viingilio siwezi kujibu chochote"

Naye Mwenyekiti Msaidizi wa Polisi Tanzania,  Robert Munisi alisema kuwa malalamiko hayo wameyasikia lakini tatizo muda sio rafiki kuwasaidia.

"Hata sisi tumefuatwa na baadhi ya watu wakidai kadi kazisomi na tumefuatilia lakini kumbe wameuziwa kadi feki huko Dar-es-salaam, hivyo hatuna msaada kwa Sasa zaidi wakashitaki kwa klabu yao wapate msaada"