Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT watamba kuendeleza ushindi kwa Yanga

Muktasari:

Timu hiyo inasaka ushindi kwenye kila mchezo ili kujinasua kwenye mstari wa kushuka daraja.

Dodoma. ILI kuendelea kuwa na matumaini ya kubaki ligi kuu, maafande wa JKT Tanzania, wamejigamba kuibuka na ushindi mbele ya Yanga, kwenye mchezo wa ligi kuu kesho Jumatano.

Kocha Abdallah Mohamed 'Bares' ametamba kuendeleza matokeo hayo ya ushindi, kufuatia kushinda mchezo uliopita dhidi ya Gwambina.

Bares amesema, Yanga wamekuja wakati mbaya ambao wao wanahitaji matokeo ya ushindi tu, jambo ambalo litawapa wakati mgumu kuwakabili.

"Tumejipanga kushinda mchezo huu, licha ya kwamba tunawaheshimu Yanga ila hatutafanya makosa zaidi ya kuwajibika kimchezo ili tuwafunge huku tukitambua kuwafunga kutatutoa chini ya msimamo" amesema Bares.

Ushindi kwa maafande hao dhidi ya Yanga utawafanya wafikishe alama 33 na kuwaondoa kwenye mstari wa njano.

Mstari huo kwa timu zilizopo nafasi ya 14 na 13, ni wa timu zitakazocheza mechi za mchujo ili zishishuke daraja.

Imeandikwa na Matereka Jalilu