Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Tanzania yatimiza ahadi ikitibua 'cleansheet' za Mashujaa

Muktasari:

  • JKT Tanzania imepata ushindi huo baada ya kucheza mechi tatu mfululizo bila ushindi ikiambulia sare moja na vichapo viwili

Mwanza. KAMA ilivyoahidi jana Jumatatu kupitia taarifa kwa umma kuitandika Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu, JKT Tanzania imefanya kweli kwa kutimiza ahadi hiyo kwa kuwachapa maafande wenzao bao 1-0.

Timu hizo zimekutana leo Oktob 3, 2023 katika mchezo wa Ligi Kuu raundi ya tano ambao umepigwa katika Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kuanzia saa 10 jioni.

Bao pekee na la ushindi katika mchezo huo limepachikwa wavuni na mshambuliaji, Edward Songo katika dakika ya 79 kwa shuti la kiufundi akiunganisha pasi ya Dany Lyanga.

Ushindi huo ni wa kwanza kwa JKT Tanzania tangu ilipoanza kuutumia Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga, ambapo imecheza michezo miwili dimbani hapo ikianza kwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar Ijumaa iliyopita.

JKT Tanzania imepata ushindi huo baada ya kucheza dakika 270 bila ushindi, ikipoteza 5-0 mbele ya Yanga, 2-1 dhidi ya KMC na 1-1 na Kagera Sugar, huku ukiwa ushindi wa pili katika mechi tano za ligi ikiifunga pia Namungo bao 1-0.

Mashujaa FC imeruhusu bao la kwanza msimu huu katika ligi kuu baada ya kucheza mechi nne sawa na dakika 360 bila wavu wake kuguswa ikishinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, 0-0 na Geita Gold, 2-0 dhidi ya Ihefu na suluhu (0-0) na Namungo FC.

Kipa wa Mashujaa FC katika mchezo wa leo, Hashim Mussa ameruhusu bao la kwanza baada ya kucheza dakika 180 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa, akipata 'Cleensheet' dhidi ya Ihefu (2-0) na Namungo (0-0), ambapo kipa huyo ameonyeshwa kadi ya njano dakika ya 69 na mwamuzi Omary Mdoe kwa kupoteza muda.

Mussa amedaka mfululizo katika mechi tatu akichukua nafasi ya Lameck Kanyonga aliyedaka mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold bila kuruhusu wavu wake kutikiswa.

Baada ya ushindi huo, JKT Tanzania imefikisha pointi saba na kupanda mpaka nafasi ya sita kutoka ya 10, huku Mashujaa FC ikibaki na pointi zao nane katika nafasi ya nne nyuma ya vinara Yanga, Azam na Simba.

Huu ni mchezo wa pili nyumbani kwa JKT Tanzania baada ya kucheza michezo mitatu mfululizo ugenini dhidi ya Yanga, Namungo na KMC, huku ukiwa mtanange wa pili ugenini kwa Mashujaa FC baada ya kumenyana na Namungo katika Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.