Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jay Msangi: Nachafuliwa kwenye ngumi

Muktasari:

  • Hata hivyo, siku chache tu baada ya malalamiko hayo, Msangi alipewa kibali cha kumpeleka bondia, Maono Ally nchini Demnark huku akiacha maswali kwa wadau wa ndondi kuhusu namna anavyopata kibali cha kusafirisha mabondia wakati amekuwa akilalamikiwa.

UKIMZUNGUMZIA mapromota wa ngumi, bila shaka Jay Msangi anatambulika haraka kutokana na kile anachokifanya kwenye mchezo huo. Hata hivyo, mwenyewe anakiri mashabiki wengi wa mchezo huo hawana imani naye, lakini hayuko hivyo anavyozungumzwa.

Si unakumbuka tukio lake la kwanza lililomtambulisha kwenye ndondi ni lile pambano la ubingwa wa dunia kati ya Francis Cheka na Phil William ambalo alimleta nchini hadi bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Frans Botha, pambano ambalo lilisababisha afungiwe.

Msangi hakuishiwa matukio baada ya kufunguliwa, ikiwamo madai ya kuwadhurumu mabondia fedha zao za mapambano na hivi karibuni Ibrahim Class alimlalamikia alipokwenda naye Afrika Kusini kwenye pambano.

Hata hivyo, siku chache tu baada ya malalamiko hayo, Msangi alipewa kibali cha kumpeleka bondia, Maono Ally nchini Demnark huku akiacha maswali kwa wadau wa ndondi kuhusu namna anavyopata kibali cha kusafirisha mabondia wakati amekuwa akilalamikiwa.

“Siko hivyo ninavyosemwa, nachafuliwa na washindani wangu ambao wamekuwa wakiunganisha ‘doti’ hasa baada ya kutokea ishu ya kushindwa kumlipa bondia Mmarekani aliyepigana na Cheka,” alisema Msangi.

Alisema wakati ule ndiyo alikuwa ameingia kwenye ngumi kwa mara ya kwanza nchini, hivyo hakuwa akijua vitu vingi, baada ya hapo mashabiki wameonekana kutomwamini.

Alisema kuna washindani wake kwenye uwakala ndiyo wanatumika kumchafua ili wamwondoe kwenye ‘reli’ katika masumbwi, kitu ambacho hakiwezekani.