Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jamhuri safii, Makata aisubiri Simba

Wakazi wa mkoa wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla hivi karibuni wataanza kushuhudia mechi za Dodoma Jiji zikichezwa usiku baada ya Uwanja wa Jamhuri unaotumiwa na timu hiyo kuendelea kuwekwa taa ndani ya uwanja na zoezi hilo likitarajia kukamilika Septemba 25.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa uwanja huo kutumika kwa mechi za usiku ambapo hata ratiba ya Ligi Kuu Bara imedhihirisha hilo kwa mechi nyingi za nyumbani za timu hiyo kupangwa kuchezwa kuanzia saa 1 usiku.

Kulingana na ratiba, Dodoma Jiji itaanza na Ruvu Shooting katika mchezo utakaofanyika Septemba 28 kabla ya siku tatu baadaye kucheza na mabingwa watetezi, Simba.

Kocha mkuu wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata amesema imekuwa afadhali kukutana na Simba mapema kuliko angekutana na mabingwa hao watetezi baadaye wakati mechi nyingi zikiwa zimeshachezwa.

Alisema kucheza mechi ya pili tu na Simba baada ya ligi kuanza itakuwa vizuri kwake kupima ubora wa kikosi chake na kufanya marekebisho katika mechi zitakazofuata.

“Nimeiona ratiba na naifanyia kazi kulingana na maandalizi ya timu kwa ujumla kuelekea ligi hiyo. Kuhusu Simba nadhani haijawa tatizo kwetu kukutana nao mapema tena uwanjani kwetu, ni vizuri kukutana nao sasa kwani itatusaidia kujua ubora wa kikosi chetu na kutuandaa vizuri kwa mechi zitakazofuata,” alisema.

Makata pia alisema kambi ya timu yake iliyokuwa mkoani Morogoro imekuwa nzuri ambayo imewapa wakati mzuri wa kujiandaa kwa utulivu kabla ya kuanza mikiki mikiki ya ligi kuu mwishoni mwa mwezi huu.

Ligi Kuu msimu huu ina mechi nyingi za usiku.