Ishu ya Mukoko, Ninja Yanga iko hivi

Mwanaspoti ambalo ndilo gazeti pekee la Tanzania lililotuma Mwandishi nchini Morocco, limewashuhudia na linaweza kuthibitisha kwamba mastaa wa Yanga, Shaibu Ninja na Mukoko Tonombe wako kwenye kambi ya Yanga mjini hapa tofauti na inavyozushwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Yanga ipo nchini Morocco kwenye kambi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Jana uongozi wa Yanga ulifafanua kwamba mastaa hao wanapewa mazoezi maalum na matibabu kama maelekezo ya benchi la ufundi yanavyotaka kabla hawajajiunga na programu ya timu nzima.
SOMA: Watatu wapya watua Yanga
Mwanaspoti linajua kwamba kabla ya Jumatatu tayari watakuwa wamerejea kwenye mazoezi ya pamoja na wenzao ambayo yameanza kunoga chini ya Kocha Nabi na jopo lake.