Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ingwe yakatiza uhusiano wa Odera KCB

Muktasari:

  • Kurejea kwa Odera, aliyefunga mabao 12 msimu jana kutapiga jeki kikosi cha kocha Andre Casa Mbungo.

STRAIKA Ezekiel Odera anatarajiwa kurejea klabu yake ya AFC Leopards kutoka KCB pindi tu dirisha fupi la uhamisho litakapofunguliwa juma lijalo.

Odera alitumwa kwa mkopo wa msimu mmoja klabu ya KCB lakini hajapata muda mwingi wa kucheza wakati Ingwe inakosa mshambulizi hatari.

“Kocha Nikola Kavazovic ndiye aliyesisitiza kwamba Odera atumwe kwa mkopo kwa sababu nyingi tu lakini tutamrejesha hivi karibuni,” alisema katibu mkuu wa Ingwe Oscar Igaida.

Leopards imefunga mabao kumi tu kwenye mechi 13 za Ligi Kuu na kujipata nafasi ya pili kutoka mwisho wa jedwali la timu 18 msimu huu.

Kurejea kwa Odera, aliyefunga mabao 12 msimu jana kutapiga jeki kikosi cha kocha Andre Casa Mbungo.

Hata hivyo, atapigania nafasi na mastraika waliopo kwa sasa, Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Wai Yeka, Vincent Oburu na Marcel Kaheza wa Tanzania.