Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ihefu FC, Majimaji wakabana koo, Gwambina yachungulia Ligi Kuu Tanzania Bara

Muktasari:

Majimaji sasa inafikisha pointi 31 sawa na Mbeya Kwanza inayoshika nafasi ya tatu na kufufua matumaini ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao kama wataendelea kupata alama tatu kwa wapinzani wao

Dar es Salaam.Ushindi wa bao 1-0 walioupata Ihefu FC mbele ya ndugu zao, Mbeya Kwanza kwenye Uwanja wa Highland Estates umezidi kukoleza vita ya kusaka kupanda daraja katika Kundi B.

Ushindi huo ulitokana na bao lililofungwa na Godfrey Kitengamlima na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 36 sawa na Dodoma FC ambayo juzi Jumapili iliichapa 2-0 African Lyon.

Kichapo hicho kwa Mbeya Kwanza kinamuongezea presha baada ya Majimaji FC kushinda 2-0 mbele Friends Rangers ambayo yalifungwa na Vicent Anthonio dakika ya 10 pamoja na Arafat Adam dakika ya 88.

Majimaji sasa inafikisha pointi 31 sawa na Mbeya Kwanza inayoshika nafasi ya tatu na kufufua matumaini ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao kama wataendelea kupata alama tatu kwa wapinzani wao.

Vinara wa Kundi B, Gwambina FC (37) inasaka pointi sita pekee kujihakikishia kucheza Ligi Kuu msimu ujao baada ya kukusanya alama hizo na kumwacha mpinzani wake Geita Gold kwa alama 10 baada ya mwishoni mwa wiki kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Arusha FC.

Kocha wa Ihefu FC, Maka Malwisi alisema watahakikisha wanapambana na kuvuna alama tatu katika michezo iliyobaki na kumuombea adui wao atereze kwenye michezo yake.

"Kila mchezo kwetu ni vita, wachezaji na viongozi wanalitambua hilo, hivyo kila mchezaji anajua kitu anachotakiwa kukifanya kwaajili ya timu yake na maisha yake kupitia soka kazi ambayo aliichagua," alisema Malwisi.

Kocha wa Majimaji FC, Peter Mhina alisema wanahitaji kurejesha heshima katika Mkoa wa Ruvuma kwa wapenzi wa soka ambao kwa misimi miwili wamekosa kusuhudia Ligi Kuu nyumbani.

'Tunayo nafasi ya kupanda Ligi Kuu na uwezo tunao wa kuhakikisha kila mchezo tunapata alama tatu ambazo ndio silaha pekee ya kutufanya kuwa na matumaini ya kurejea Ligi Kuu," alisema Mhina.