Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Asec aingia anga za Simba

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Simba iliyosaliwa na mechi tatu inazohitaji ushindi ili kutangaza ubingwa msimu huu baada ya kuusotea kwa misimu mitatu mfululizo, imeendelea na mipango ya kukisuka kikosi kipya ikihamishia nguvu kwa mshambuliaji matata Celestin Ucua wa Asec Mimosas ya Ivory Coast ili kuja kuchukua nafasi ya Leonel Ateba anayeelezwa huenda akapigwa chini.

SIMBA inajiandaa kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya KenGold itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora, lakini mabosi wa klabu hiyo wanaendelea kupiga hesabu za kuboresha kikosi wakianza mazungumzo na straika wa Asec Mimosas.


Simba iliyosaliwa na mechi tatu inazohitaji ushindi ili kutangaza ubingwa msimu huu baada ya kuusotea kwa misimu mitatu mfululizo, imeendelea na mipango ya kukisuka kikosi kipya ikihamishia nguvu kwa mshambuliaji matata Celestin Ucua wa Asec Mimosas ya Ivory Coast ili kuja kuchukua nafasi ya Leonel Ateba anayeelezwa huenda akapigwa chini.


Simba imeamua kurudi tena Asec ili kumbeba mshambuliaji huyo mwenye miaka 23 anayejua kufunga mabao kwani msimu huu akicheza kwa mkopo kutoka Zoman FC tangu Januari 2025  amemaliza na mabao saba na asisti nne katika Ligi Kuu timu hiyo ikimaliza ya pili. Katika mechi za kimataifa Asec ikiishia robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Ecua alifunga mabao mawili, huku akisifiwa kwa umahiri wa kupiga penalti za panenka na anayeweza kutokea pembeni ya uwanja.

Inaelezwa kuwa, Simba imekuwa ikimfuatilia Ecua kupitia michuano ya Kombe la Shirikisho ya msimu huu iliyoishia robo fainali kwa kutolewa na RS Berkane ya Morocco waliobeba taji kwa kuizidi ujanja Wekundu iliyocheza nao fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.

Taarifa kutoka ndani ya Simba ni kwamba mabosi wa klabu hiyo kwa sasa wapo katika mazungumzo na wasimamizi wa mshambuliaji huyo baada ya kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids kuridhika na ubora wa nyota huyo aliyezaliwa Januari 1, 2002.

Ecua alimaliza nafasi ya pili ya vinara wa mabao wa ASEC nyuma ya Salifou Diarrassouba aliyefunga manane na hesabu za Simba ni kumleta Msimbazi ili kumaliza tatizo la mabao licha ya kuwepo kwa nyota wawili waliosajiliwa msimu huu Steven Mukwala na Ateba, mbali na mzawa Valentino Mashaka.

Taarifa zinasema sababu kubwa zilizomshawishi kocha Fadlu kufungua mazungumzo na mshambuliaji ni akili yake ya kufunga pamoja na ubora wa kumiliki mpira ambazo Ecua anao.

"Ni mshambuliaji mzuri ana nguvu na kimo kizuri, lakini anajua sana kufunga ambalo hilo ndio muhimu tulianza kuifuatilia wakati tu anatua asec," alisema bosi huyo.

"Bado hatujamsainisha, lakini tunazungumza na wasimamizi wake wakati huo huo tunaendelea kupokea taarifa kutoka kwa maskauti wetu sehemu mbalimbali.

"Tunataka kumaliza haraka hesabu za kutafuta wachezaji bora hasa hawa washambuliaji kabla kukutana na wakati mgumu."


CELESTIN ECUA

Nyota huyo mwenye miaka 23 kiasili ni mshambuliaji wa pili katika mfumo wa 4-4-2 kwani huyu ni ball to feet player, ila kwenye mfumo wa 4-2-3-1 na 4-3-3 anaweza kutokea pembeni kama winga.

Sifa kubwa ni uwezo kwa kufunga mabao kwa miguu yote miwili na pia kutumia kichwa, huku ikielezwa ni fundi wa mikwaju ya penalti kwa staili ya panenka na katika michuano ya CAF ya msimu huu alifunga mabao mawili, wakati katika Ligi Kuu ya Ivory Coast alifunga saba na kuasisti nne.

Iwapo dili la kutua Msimbazi litatiki kutakuwa na maana ya mmoja katia ya Mukwala au Ateba kumpisha katika nafasi hiyo, huku karata ikimuangukia zaidi Ateba ambaye licha ya kupewa muda mwingi na kocha Fadlu, ameshindwa kuwa na maajabu japo kwa sasa ana mabao 12 akilingana na Mukwala, lakini nusu ya mabao hayo yametokana na penalti akilingana na Jean Charles Ahoua