Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu ndiyo muonekano wa jezi mpya ya Pamba Jiji

KLABU ya Pamba Jiji FC imezindua jezi zake za msimu wa mwaka 2023/2024 na duka lake litakalouza jezi pamoja na duka linalotembea (mobile shop) ambapo kila jezi moja itakayouzwa (Sh30,000) klabu hiyo itapata Sh8,000.

Jezi hizo ambazo zimetengenezwa na kampuni ya Netsport zimezinduliwa leo Oktoba 6, 2023 saa 3 usiku katika jengo la Rock City Mall ambapo pia duka la timu hiyo litapatikana hapo.

Jezi ya nyumbani ni ya rangi ya kijani yenye ufito mweupe shingoni na kwenye mikono, jezi ya ugenini ni ya rangi nyeupe yenye michirizi ya kijani na jezi ya tatu ni ya rangi ya blue (rangi ya halmashauri ya Jiji la Mwanza) yenye ufito mweupe shingoni na kwenye mikono

Akizindua jezi hizo, Meya wa halmashauri ya Jiji la Mwanza, Constantine Sima amesema uzinduzi wa jezi hizo utachangia kuinua uchumi wa timu yao huku akiwataka mashabiki wa klabu hiyo kote nchini kununua kwa wingi jezi hizo ili kuchangia mapato ya klabu.

"Huu ni mwanzo wa safari kubwa ya timu yetu ya Pamba ambao tumekuwa tukiukusudia, tunao mashabiki na wapenzi wa timu ya Pamba kote nchini ushabiki huu uwe wa vitendo tununue jezi na kuiunga mkono Ili tufikie dhamira kubwa ambayo kila mwana Mwanza anatamani kuiona," amesema Sima

Mmoja wa Wakurugenzi wa Netsport, Darius Bujaga amesema hatua hiyo ni safari ya kufanya mapinduzi ya mpira wa miguu kwa klabu hiyo yenye heshima nchini na inastahili kuwa mahali fulani kwa sasa.



"Sisi tulivyoona klabu hii inasuasua huko chini tukaona tuje na kitu cha kuisapoti tukadhamini vifaa vya michezo tuliona tusiisubiri mpaka ipande tukaona tuifute kule iliko na tutapanda nayo kwahiyo tumejizatiti kabisa kufanya kazi kubwa katika kuwavalisha kwa ubora mkubwa, tumewaandalia bidhaa bora kabisa na hamtojutia," amesema



Mtendaji Mkuu wa Pamba Jiji, Alhaji Majogoro katika mauzo ya jezi hizo (Sh30,000) klabu hiyo itapata mgao wa Sh8,000 ambapo 

amewaomba wadau na mashabiki kununua jezi kwa wingi kuichangia timu hiyo, huku akitamba kuwa kiasi hicho ni kikubwa kuwahi kutolewa na timu kwenye soka nchini.

"Wito wangu kwa wapenzi na mashabiki wa Pamba tuendelee kushikamana Kwa kila hali kuhakikisha Pamba inarejea ligi kuu, tusibaguane huyu anatoka mkoa mwingine, tupeane ushirikiano tufanye kazi kwa pamoja naamini wakati huu hakuna wa kutusimamisha tunakwenda Ligi Kuu na tutaileta Ligi Kuu Mwanza," amesema Majogoro

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Peter Juma amesema "Tunatoa wito kwa wafadhili wengine milango bado Iko wazi, tukishikana pamoja timu yetu itapanda daraja,"