Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ndoa ya Ali Kiba si mchezo mchezo aisee

Muktasari:

  • Hata hivyo, habari mbaya kwa mashabiki hao ni kuwa, Kiba anafunga ndoa na mrembo Amina Khaleef, ambaye makazi yake yapo Mombasa, Kenya. Wengi walikuwa na shauku kuona Kiba anafunga ndoa na kuanzisha familia na mpenzi wake wa muda mrefu, Jokate Mwegelo.

KAMA huna kadi ya mwaliko basi pole yako, habari njema ni kuwa mkali wa Bongo Flava, Ali Kiba, anafunga ndoa rasmi Aprili 19, mwaka huu, mjini Mombasa. Ndoa hiyo itakuwa imekata kiu ya mashabiki waliokuwa wakitamani kumuona Kiba, anavuta jiko kama ilivyokuwa kwa Ambwene Yesaya ‘AY’ na Hamis Mwinyijuma ‘Mwana FA’.

Hata hivyo, habari mbaya kwa mashabiki hao ni kuwa, Kiba anafunga ndoa na mrembo Amina Khaleef, ambaye makazi yake yapo Mombasa, Kenya. Wengi walikuwa na shauku kuona Kiba anafunga ndoa na kuanzisha familia na mpenzi wake wa muda mrefu, Jokate Mwegelo.

Habari za kuaminika zinasema kuwa, mchakato wa ndoa hiyo imekamilika na amsha amsha nyumbani kwa bibi harusi mtarajiwa zimeanza kupamba moto.

Mwanaspoti linafahamu kuwa, kwa sasa Kiba yuko nchini China kukamilisha baadhi ya mambo ikiwepo kununua samani za nyumba yake aliyojenga Tabata, Dar es Salaam.

Pia, inafahamika kuwa mipango ya harusi hiyo imekuwa ikiratibiwa kwa usiri mkubwa na rafiki wa karibu na Kiba, Sultan Joho ambaye ni Gavana wa Mombasa.

Chanzo chetu kimeeleza kuwa, ndugu na jamaa wa Kiba walitarajiwa kuanza kuwasili mjini Mombasa jana, na ndoa hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na watu wachache.

“Mambo yanakwenda vizuri kule Mombasa na Kiba atafunga ndoa Aprili 19, kisha sherehe nyingine itafanyika Dar es Salaam Aprili 29. Jamaa alisafiri kwenda Uchina lakini kwa sasa anaweza kuwa Dar, alikwenda kukamilisha manunuzi ya samani za ndani ili mwali atakapoingia ndani kila kitu kiwe tayari. Chini ya Joho (Sultan) kila kitu kinakwenda vizuri, unajua hawa watu ni marafiki sana,” kilisema chanzo chetu.

Hivi karibuni mkali mwingine wa Bongo Flava, Ambwene Yesaya a.k.a AY alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku, ambapo alifanya sherehe mbili moja kule Rwanda na nyingine Tanzania.