Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hazard aaga, awapa zawadi Chelsea

Muktasari:

  • Kiungo wa pembeni wa Chelsea, anaondoka katika klabu hiyo akiwa shujaa baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Europa dhidi ya Arsenal.

 

Baku. Eden Hazard amefunga mabao mawili na kuipa Chelsea  ubingwa wa Kombe la Europa katika mchezo wa fainali uliochezwa jana usiku ambao timu hiyo ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Arsenal.

Mabao ya Hazard yalikuwa ni zawadi ya mwisho kwa mashabiki wa Chelsea kwenye Uwanja wa Olimpiki, kwani baada ya mchezo kumalizika aliaga rasmi.

Nahodha huyo wa Ubelgiji anatarajiwa kutia saini mkataba wa kujiunga na Real Madrid katika majira ya kiangazi kwa kitita kinachokadiriwa kuwa Pauni115 milioni.

“Kwaherini. Nilifanya uamuzi wa kuondoka wiki mbili zilizopita sasa ni jukumu la klabu zote mbili. N mimi kama mashabiki nasubiri kuona nini kitatokea siku chache zijazo,” alisema Hazard.

Mchezaji huyo alisema ndoto yake ilikuwa ni kucheza Ligi Kuu England na amecheza miaka saba, lakini huu ni muda mwafaka wa kuondoka kwenda kupata changamoto mpya.

Hazard anaondoka Chelsea akiwa na rekodi ya kufunga mabao 110 katika mechi 352 alizocheza na kutoa pasi za mwisho 92.

Mbali na Hazard aliyefunga mabao yake dakika ya 65 na 72, mengine yaliwekwa wavuni na mshambuliaji nguli Olivier Giroud dakika ya 49 na Pedro (60). Bao la Arsenal lilifungwa na Alex Iwobi dakika ya 69.

Wakati Hazard akimaliza vyema Chelsea, kipa mkongwe wa Arsenal, Petr Cech alitoka uwanjani akiwa na uchungu baada ya kufunga mabao manne ikiwa ni mechi yake ya mwisho kwa kuwa tayari alishatangaza kustaafu.