Hans Poppe akumbukwa mkutano Simba

Sunday November 21 2021
Poppe PIC
By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Simba, Zacharia Hans Poppe amekumbukwa kwenye mkutano mkuu wa klabu ya Simba unaoendelea Dar es Salaam.

Wanachama wa klabu hiyo wamesimama kwa dakika moja kumuombea Poppe aliyefariki miezi kadhaa zilizopita na kuzikwa kwao Iringa.

Poppe aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo enzi za uhai wake anakumbukwa kwa kujitoa kwake kwenye kitengo hicho.

Mbali na Poppe, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah 'Try Again' amesema mbali na Poppe pia wanamkumbuka mama wa Barbara Gonzalez na wanachama wote wa klabu hiyo waliotangulia mbele za haki.

Advertisement