Hamisa Mobetto ndani ya uzi wa Wydad

Muktasari:
- Hamisa alikuwa uwanjani jana wakati Wydad ikivaana na FC Porto, ambapo Aziz Ki kuingia uwanjani kwa mara ya kwanza kuitumikia timu hiyo iliyopoteza kwa bao 1-0 kisha mwanamitindo huyo aliandika jumbe kwa akaunti yake ya instagram.
SIKU chache tangu, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga anayekipiga Wydad Casablanca ya Morocco, Stephane Aziz KI, mkewe ambaye ni mrembo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto ametupia picha kadhaa akiwa ametinga uzi wa klabu hiyo ya Morocco.
Hamisa alikuwa uwanjani jana wakati Wydad ikivaana na FC Porto, ambapo Aziz Ki kuingia uwanjani kwa mara ya kwanza kuitumikia timu hiyo iliyopoteza kwa bao 1-0 kisha mwanamitindo huyo aliandika jumbe kwa akaunti yake ya instagram.
"Ninajivunia sana kumshangilia mume wangu @wacofficiel nikiwa jukwaani – kwa kweli hakuna sehemu nyingine ningependelea kuwa."
Haya maneno ni ya upendo, kujivunia, na msaada kwa mume wake Aziz KI pindi anapoingia uwanjani.
Aziz Ki jana kaingia uwanjani kwa mara ya kwanza akitokea benchi akiwa na uzi wa Wydad Casablanca iliyopasuka mbele ya wababe hao wa Ureno.