Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtasingwa kiroho safi Azam

MUTASINGWA Pict

Muktasari:

  • Azam iliyoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ilitolewa katika raundi ya kwanza na APR ya Rwanda, kisha ikang’olewa hatua ya 32 Bora mbele ya Mbeya City katika Kombe la Shirikisho (FA), huku ikipoteza kasi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikishika nafasi ya tatu kwa sasa katika msimamo.

KIUNGO mkabaji wa Azam FC, Adolf Mtasingwa amesema licha ya timu hiyo kushindwa kufikia malengo kwa msimu huu ikiwamo kung’olewa mapema katika Kombe la Shirikisho (FA) na ile ya CAF, kwa upande wake ulikuwa msimu bora.

Azam iliyoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ilitolewa katika raundi ya kwanza na APR ya Rwanda, kisha ikang’olewa hatua ya 32 Bora mbele ya Mbeya City katika Kombe la Shirikisho (FA), huku ikipoteza kasi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara ikishika nafasi ya tatu kwa sasa katika msimamo.

Hata hivyo, Mtasingwa aliyekuwa akitajwa kuviziwa na Yanga, amesema kama wachezaji wanajisikia vibaya kukwama kuifikisha timu katika malengo, hata hivyo anachoshukuru amekuwa na msimu mzuri japo ameishia njiani kutokana na kupata majeraha.

Mara ya mwisho kucheza kwa kiungo huyo ambaye amekuwa muhimu katika kikosi cha kwanza ilikuwa Februari 15 mwaka huu dhidi ya Mashujaa ambapo Azam ilishinda 2-0 mechi ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mtasingwa alisema licha ya kushindwa kumaliza msimu anaamini kuwa alikuwa na msimu bora na malengo binafsi yametimia isipokuwa alishindwa kuipambania timu hiyo kufikia ilikotamani.

“Tumepoteza mataji yote tuliyokuwa tunayapigia hesabu, hayakuwa malengo yetu. Lakini tumejifunza kutokana na makosa kwani tulianza vizuri msimu, ila mambo yakabadilika katika duru la pili ambalo tulipoteza mechi nyingi hiyo ndio ilikuwa shida. Tutarudi kujipanga msimu ujao, tumejua wapi tulikosea,” alisema Mtasingwa na kuongeza;

“Tuna timu bora na shindani, kila kitu kinawezekana, naamini mechi mbili zilizobaki timu itafanya vizuri na kuendelea kubaki katika nafasi ya tatu tulipo sasa japo hayakuwa malengo yetu.”

Akizungumzia msimu kwa ujumla alisema ni msimu bora na wa ushindani kilichotokea hasa kwa timu zilizoshuka daraja hakuna aliyetarajia hayo na anaamini kuna ushindani bado unaendelea katika mechi mbili zilizobaki.

“Huu ulikuwa msimu dume ukiangalia hata ubingwa hautapatikana kirahisi kutokana na timu kupishana alama ndogo na ubingwa kuamuliwa na mchezo wa mwisho tofauti na misimu mingine iliyopita ambapo bingwa alikuwa anajulikana zikiwa zimebaki mechi zaidi ya tatu au nne.”

Tangu aumie, kiungo huyo amekosekana katika mechi nane na kati ya hizo Azam imeshinda tatu sare tatu na vipigo viwili. Matokeo yalikuwa: Coastal Union 0-0, Simba 2-2, Namungo 1-1, ushindi dhidi ya Tanzania Prisons 4-0, KenGold 2-0, Kagera Sugar 4-2 wakati vipigo ni dhidi ya Yanga 2-1 na dhidi ya Singida Black Stars 1-0.