Hali sio shwari kwa Yanga kuwakosa Mayele, Kibwana...

WAKATI mashabiki wa Yanga wakifurahia kurudi kwa Heritier Makambo klabu hiyo imetoa taarifa ambayo sio nzuri sana kwa mashabiki wao.
Makambo jana aliisaidia timu yake kutinga hatua ya 36 bora kombe la Shirikisho wa kuifungia mabao matatu kwenye ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Ihefu katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Uongozi wa Yanga leo Alhamisi umetoa taarifa ya kuthibitisha kukabiliwa na majeruhi kwa wachezaji kuongezeka ndani ya kikosi chao kwa kutaja majina ya mastaa wanne ambao watakuwa nje ya Uwanja kwa muda.
Taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa na idara ya habari inasema mastaa wake Kibwana Shomari, Yusuf Athuman, Fiston Mayele na Yacouba Sogne ambaye ni majeruhi wa muda mrefu.
“Uongozi unafanya jitihada za kuwapatia matibabu Shomari, Athuman nje ya nchi kutokana na matatizo waliyonayo lakini kwa upande wa Mayele anaendelea vizuri na matibabu na Sogne aliyekuwa nje anaendelea vizuri,” ilisema taarifa hiyo.
Yanga ambayo inatarajia kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons ugenini Jumapili na itawakosa nyota hao.