Goti lampeleka Ndunda kutibiwa India

Dar es Salaam. Kipa wa Simba, Said Mohamed Ndunda ataondoka kwenda nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya goti lake linalomsumbua anataraji kuwa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi sita.
Kwa mujibu wa taarifa ya Simba iliyotolewa na Afisa Habari wake Haji Manara ilisema Nduda aliumia mazoezini wakati timu ikijiandaa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga wiki iliyopita,
Matibabu hayo yatamuweka mchezaji huyo nje ya uwanja kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kujiunga tena na wenzake kwa ajili ya mazoezi na anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa wiki hii.
Klabu pia inayofuraha , kuwaambia kuwa wachezaji wake John Bocco na Haruna Niyonzima, ambaye alipata majeraha madogo juzi wameshaanza mazoezi na wenzao hii leo.
Huku pia Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu naye anatarajiwa kuanza mazoezi siku chache zijazo baada ya madaktari kuthibitisha uzima wa afya yake.
Mwisho,Klabu inaufahamisha umma wa watanzania kupitia vyombo vya habari kuwa taarifa zote rasmi za klabu ya Simba zitakuwa zikitolewa katika mfumo na barua hii(Heading paper)
Pia Klabu inawaomba washabiki wake kote nchini kuendelea kuiunga mkono timu yao ili iendelee kufanya vizuri kwenye ligi kuu iliyoaanza wikiendi iliyopita.