Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gaucho anukia umeneja Simba Queens

GAUCHO Pict

Muktasari:

  • Gaucho aliyehudumu kikosini hapo kwa takribani misimu nane kwa sasa tangu alipojiunga akitokea Mlandizi Queens iliyoweka heshima ya kuwa timu ya kwanza kubeba ubingwa wa WPL. kisha kwenda Morocco kucheza soka la kulipwa kabla ya kurejea kuendelea kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi.

MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), Simba Queens imepanga kumpa heshima mshambuliaji mkongwe wa timu hiyo, Mwanahamisi Omary 'Gaucho' kwa kumtunuku cheo cha umeneja wa timu.

Gaucho aliyehudumu kikosini hapo kwa takribani misimu nane kwa sasa tangu alipojiunga akitokea Mlandizi Queens iliyoweka heshima ya kuwa timu ya kwanza kubeba ubingwa wa WPL. kisha kwenda Morocco kucheza soka la kulipwa kabla ya kurejea kuendelea kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi.

Ndani ya misimu hiyo aliisaidia Simba kuipa ubingwa wa WPL mara nne na kuwa mchezaji pekee aliyeweka rekodi ya kufunga hat-trick katika dabi na kufunga mabao 10 kwenye mechi 13 walizokutana Simba Queens na Yanga Princess.

Mmoja wa kiongozi wa Simba (jina tunalo) aliliambia Mwanaspoti kuwa wameona nyota huyo umri umeenda hivyo wamepanga kumpa heshima ya kuwa meneja kwenye klabu kutokana na kile alichokifanya ndani ya misimu.

"Hakuna asiyemfahamu Gaucho amefanya makubwa sana akiwa na Simba na Twiga Stars, bado ni mchezaji mzuri lakini kutokana na umri hawezi kuendana na kasi ya ligi kwa sasa ligi imekuwa ngumu," alisema kiongozi huyo na kuongeza

"Hivyo viongozi tumekaa na kuona ni jambo zuri kumfanyia kitu kutokana na heshima aliyotupa ndani ya kipindi chote lakini inavyoonekana tangu tumpe wazo hilo hajarudisha majibu ni kama hataki hivi."

Mbali na hilo Mwanaspoti linafahamu kuwa mshambuliaji huyo anatamani kuendelea kucheza akiamini ana uwezo kama ilivyokuwa kwa John Bocco ambaye alipewa nafasi ya kuwa kocha wa timu ya vijana na baadae akatimkia JKT Tanzania kuendelea kusakata kabumbu.

Hata hivyo, gazeti hili linafahamu kuwa Gaucho ana ofa kutoka timu mbalimbali za nje ya nchi hivyo kuna uwezekano kama hataendelea kucheza Simba huenda akaibukia nje.