Gamondi amuanzisha Guede badala ya Mzize

KOCHA wa Yanga Miguel Gamondi, ameanza na asilimia kubwa ya wachezaji waliocheza mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi, isipokuwa Clement Mzize pekee.

Kwenye mchezo wa leo badala ya Gamondi kumuazisha Mzize nafasi yake ameichukua Joseph Guede ambaye kwenye mchezo wa Dar es Salaam aliingia kipindi cha pili.

Kikosi cha Yanga hakina mabadiliko mengine yoyote, Pacome Zouzoua na Khalid Aucho ambao wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha kwa wiki kadhaa sasa, hawapo hata kwenye benchi kama ilivyokuwa mchezo wa kwanza.

Gamondi ameanza na kipa Djigui Diarra, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Jonas Mkude ameanza kwenye mchezo wa pili mfululizo, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahaya, Guede, Stephen Aziz Ki na Kennedy Musonda.

Yanga iliizuia Mamelodi katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Mkapa na kutoka nayo suluhu na leo inatakiwa kupata ushindi au sare ya mabao ili ifuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza katika historia yao.