Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain Gate yaleta Mmisri kwa Ulimboka

Dodoma. MATOKEO mabovu kwenye Ligi ya Championship msimu huu, yamewalazimu mabosi wa Fountain Gate FC, kuleta kocha kutoka nje ya nchi.

Kocha Ahmed Soliman kutoka nchini Misri, ndiye hatimaye amekabidhiwa jukumu la kuinoa timu hiyo, akichukua nafasi ya Ulimboka Mwakingwe, aliyesitishiwa mkataba wake.

Mwakingwe aliyekua amechukua mikoba ya kuinoa timu hiyo mikononi mwa Denis Kitambi, ambaye alianza msimu kabla ya kushindwa kufikia malengo, akaondolewa na sasa imekua kwake Ulimboka.

Taarifa ya mtendaji mkuu wa timu, Fikiri Mahiza imeeleza kuwa, Kocha Soliman ameanza rasmi majukumu ya kuinoa timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu.

Mkurugenzi wa timu hiyo, Japhet Makau ameliambia Mwanaspoti kuwa, wameamua kumkabidhi kazi ya kuwapeleka ligi kuu Kocha huyo kutoka Misri, bila kujali msimamo ulivowakalia vibaya.

"Ni kweli, huyo ndiye Kocha wetu mpya kama ilivyoelezwa, tunaamini atatufikisha pale malengo yetu yalipo siku zote, bado tunaamini tuna nafasi ya kupanda ligi kuu" alisema Makau.

Kazi kubwa aliyonayo Kocha Soliman, ni kuitoa kwenye nafasi ya tisa ilipo timu hiyo yenye alama 22, ikiwa ni pungufu ya alama 20 na 21 dhidi ya timu za DTB na Ihefu zinazoongoza mbio za kupanda ligi kuu.