Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain Gate yaizima Stand United kwao

SHY Pict

Muktasari:

  • Timu za Ken Gold na Kagera Sugar zimeshashuka daraja msimu huu, huku Mtibwa Sugar na Mbeya City zikipanda kutoka Ligi ya Championship.

Fountain Gate imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United kwenye mchezo uliojaza mashabiki wengi.

Fountain imefika hapa baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 14 ambapo ilicheza mchezo wa kwanza wa mtoano na Prisons na kupoteza kwenye matokeo ya jumla.

Ushindi huu una maana kuwa sasa Fountain inatakiwa kupata angalau sare tu nyumbani kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa ili kubaki Ligi Kuu Bara kwa ajili ya msimu ujao wa 2025/ 2026.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarange Mkoani Shinyanga Fountain ilijipatia mabao kupitia kwa Kassim Shaaban, Sadic Said, Mudric Shehe, huku lile la Stand likipatikana baada ya beki Joram Mgeveke kujifunga.  

Sasa timu hizo zitarudiana kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Julai 8, mwaka huu ambao itakuwa mechi ya mwisho ya mtoano msimu huu.

Timu za Ken Gold na Kagera Sugar zimeshashuka daraja msimu huu, huku Mtibwa Sugar na Mbeya City zikipanda kutoka Ligi ya Championship.