Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain Gate yagoma kushuka daraja Bara

FOUNTAIN Pict

Muktasari:

  • Aidha, Makau amesema timu yake ya vijana umri chini ya miaka 20 ilistahili kuwa bingwa, huku akitaja bao la ushindi la Azam FC lilikuwa ni la utata.

MKURUGENZI wa Fountain Gate Academy, Japhet Makau, amesema mechi mbili zilizobaki zinaipa nafasi timu hiyo kutokushuka daraja kutoka Ligi Kuu.

Fountain Gate imesaliwa mechi dhidi ya Coastal Union inayopigwa keshokutwa Jumatano na ile ya Juni 22 itakapokuwa wageni wa Azam FC.

Aidha, Makau amesema timu yake ya vijana umri chini ya miaka 20 ilistahili kuwa bingwa, huku akitaja bao la ushindi la Azam FC lilikuwa ni la utata.

Makau aliyasema hayo hayo mchana huu, baada ya Fountain Gate, pamoja na Chama cha Madaktari wa Michezo Tanzania (TMSA) kuingia makubaliano rasmi na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika kuanzisha na kusimamia Programu ya Moyo kwa wanamichezo.

Makau alisema timu hiyo, licha ya kushika nafasi ya 14 kwa sasa, lakini haitocheza play-off kwq kuamini itafanya vizuri katika mechi mbili zilizobaki, huku akiweka wazi kuwa watacheza Ligi ya msimu ujao wakirudi wakiwa imara zaidi kwa kuwa na timu shindani.

“Tuna timu nyingi za madaraja tofauti ya umri hivi karibuni tumecheza fainali na timu ya vijana chini ya miaka 20, tulistahili ubingwa bao la utata limetufanya tumalize nafasi ya pili na kuhusu Fountain Gate katika Ligi Kuu Bara nawaambia hatuchezi play-off, tukutane msimu ujao.”

Akizungumzia ushirikiano wao na JKCI alisema ni fursa nzuri kwa klabu hiyo kuwalinda wachezaji,  huku akiwatoa hofu wazazi kuwa sasa watoto wapo mikono salama watapata vipimo kabla ya kuingia michezoni.

“Mungu ametusaidia kwa miaka yote nane tuliyoanzisha shule zetu hatujawahi kupata majanga kwa wachezaji, hivyo hatutaki kusubiri kwa kuomba Mungu tumeamua kuingia makubaliano ili kulinda afya za wanamichezo wetu,” alisema Makau na kuongeza;

“Naamini vijana wetu wote watapata fursa ya kutazamwa afya zao wazazi ambao watoto wao wanashiriki michezo waondoe hofu kabisa kwa sababu kabla ya mazoezi watakuwa wanapimwa kabla ya mazoezi na hata michezo ili kulinda afya ya wanamichezo.”

Wakati huo huo, aliwaombea futsa wanafunzi ambao pia ni wachezaji waweze kupatiwa elimu ya namna ya kujikinga na shida ya moyo kwa sababu wao pia wana ndoto ya kuwa madaktari.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu JKCI, Dk Angela Muhozya amesema makubaliano hayo yanalenga kufanya uchunguzi wa awali wa moyo kwa wachezaji wa Fountain Gate FC pamoja na wanafunzi wa shule zao zote ambazo zipo 15 kwa ujumla katika miko mbali mbali ya Tanzania ambapo wanashiriki katika shughuli za michezo mbalimbali ikiwamo mpira wa miguu.

“Mpango huu wa kuanzisha sports cardiology program inayohusisha Pre-Participation Cardiac Screening kwa wanamichezo ni hatua muhimu katika kuhakikisha usalama wa wanamichezo wetu nchini. Lengo ni kubaini mapema matatizo ya moyo ambayo yanaweza kuwa hatari na yasiyoonekana kwa macho, ili kuyazuia kabla hayajasababisha madhara makubwa,” amesema Dk Angela na kuongeza;

“Hii ni pamoja na kuzuia vifo vya ghafla vya moyo (Sudden Cardiac Death), ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa duniani kote kwa wanamichezo, hata wale waliokuwa wakionekana kuwa na afya njema.”

Amesema programu hiyo ni mpya na ya kipekee ikiwa ni sehemu ya upanuzi wa huduma zetu za kinga katika jamii, wamekuwa wakitoa matibabu ya hali ya juu, lakini sasa wanajikita zaidi katika kuzuia matatizo kabla hayajatokea, hasa kwa vijana wanaoshiriki michezo.