Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba yake Ally Mayay afariki dunia kwa ajali Tabora

BABA Pict

Nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay Tembele, amepata msiba baada ya leo Juni 16, 2025 kufiwa na baba yake mzazi.

Mhasibu wa Chama cha Wachezaji wa Zamani Tanzania (Galacticos), Idd Moshi, ameliambia Mwanaspoti kuwa baba wa staa huyo anayejulikana kwa jina la Moshe Tembele, amefariki kwa ajali ya treni baada ya kugongwa wakati akivuka eneo la Chuo cha Reli mkoani Tabora.

"Mzee wetu kafariki leo na taarifa imetolea katika chama chetu cha Galacticos, hivyo mipango ya mazishi itatolewa baada ya Mayay kufika Tabora," amesema na kuongeza.

"Amepata ajali ya treni, hivyo ni kifo cha ghafla ndiyo maana hatuwezi kusema mipango ya mazishi itafanyikaje, ila naamini Mayay akifika ndipo tutakapojua mipango inakwendaje na tutapeana taarifa nyingine zaidi."