Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fountain Gate, Tabora zimepishana kidogo tu

FOUNTAIN Pict

Muktasari:

  • Tukawaona jamaa zetu wa kule Babati, Manyara, Fountain Gate wapo katika nafasi ya 14 kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 29 katika mechi 28 ilizocheza hadi sasa ikipata ushindi mara nane na kutoka sare tano na mechi 15 imezipoteza.

KIJIWENI kwetu hapa tulikuwa tunautazama msimamo wa Ligi Kuu Bara wakati huu ambao zimebaki raundi mbili msimu wa 2024/2025 umalizike.

Tukawaona jamaa zetu wa kule Babati, Manyara, Fountain Gate wapo katika nafasi ya 14 kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 29 katika mechi 28 ilizocheza hadi sasa ikipata ushindi mara nane na kutoka sare tano na mechi 15 imezipoteza.

Mwanzoni mwa msimu walikuwa moto wa kuotea mbali na kumbuka waliwahi hadi kuwemo katika nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi nne tu za mwanzo za ligi.

Ghafla leo wapo katika nafasi ambayo kikanuni wakimaliza msimu huku wakiwepo hapo, watalazimika kucheza mechi za mchujo ili kupigania kubaki Ligi Kuu na mambo yakienda ndivyo sivyo maana yake msimu ujao tunaweza kuwaona katika Ligi ya Championship.

Duru la pili wamepata ushindi katika mechi chache na michezo mingi wamepoteza pointi kwa kufungwa au kutoka sare.

Ni kama Tabora United ambayo baada ya kupitia kipindi fulani cha raha mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, mambo yanaonekana kuwaendea kombo na sasa wanaporomoka taratibu kutoka nafasi za juu kwenda chini.

Timu zote hizo mbili msimu huu zinaongoza kwa kubadilisha makocha kutokana na sababu tofauti na kila moja hadi sasa imeshafundishwa na makocha wakuu wanne tofauti na mambo hayajatengamaa.

Mabadiliko ya makocha kwa timu nyingi za daraja la Tabora United na Fountain Gate huwa yanakuja na athari hasi ambazo mwishowe zinaigusa timu kwa vile wachezaji huchukua muda mrefu kuzoea mbinu na falsafa za makocha wapya.

Mwenendo usioridhisha wa mechi nyingi za mzunguko wa pili kwa Tabora United na Fountain Gate ni jambo ambalo halijatokana na bahati mbaya.