Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fiston: Hawa Jamaa wepesi

STRAIKA mpya wa Yanga, Fiston Abdulrazack amewataka mashabiki wa timu hiyo kukaa mkao wa kula kushangilia mabao yake kwa vile anafahamu vizuri udhaifu na uimara wa mabeki wanaocheza katika Ligi Kuu hapa nchini.

Fiston aliyenaswa na Yanga katika dirisha dogo la usajili, alisema kuwa anafahamu deni alilonalo kwa mashabiki, viongozi na wadhamini wa Yanga na atahakikisha analilipa kwa kuifungia mabao kutokana na uzoefu mkubwa alionao wa soka la Afrika na hata la hapa nchini.

“Sitaki kuongea maneno mengi bali nataka vitendo ndio vizungumze zaidi. Yanga ni timu kubwa na mashabiki wanahitaji kuona inafanya vizuri hivyo nafahamu kazi iliyonileta hapa na nini mashabiki wanategemea kutoka kwangu.

Binafsi naamini kwa ushirikiano ninaoupata kutoka kwa wenzangu, nitaweza kupachika mabao mengi na kuisaidia timu kufanya vizuri na kutimiza malengo iliyojiwekea kwani nimekutana na wachezaji wazuri hapa ambao wana ubora wa hali ya juu,” alisema Abdulrazack.

Alisema suala la ugeni katika Ligi Kuu Tanzania Bara halimpi wasiwasi kwani amekuwa akiifuatilia kwa muda mrefu na mara kadhaa ameshakutana na mabeki wake.

“Sio mara moja nimekutana na mabeki wa Kitanzania. Nilikuja hapa na timu ya Taifa ya Burundi katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia nikafunga bao ingawa Taifa Stars ilishinda kwa penati lakini pia nimeshawahi kukutana nao katika mashindano ya Chalenji kule Kenya na nikafunga pia.

Hivyo wengi wao ninawafahamu vyema ubora na udhaifu wao lakini siwezi kuusema kwa sababu kwa kufanya hivyo nitakuwa nawashtua na kuwafanya wajipange ili kunidhibiti.

Mimi nawasubiria tu uwanjani ili nitumie vyema huo udhaifu wao, kuweza kuifungia mabao ya kutosha timu yangu. Ila kikubwa wanatakiwa kujipanga,” alisema mshambuliaji huyo.

Abdulrazack alisajiliwa na Yanga katika kipindi cha dirisha dogo la usajili lililomalizika Januari 15 akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na timu ya ENPPI ya Misri ambayo pia anachezea Himid Mao wa Tanzania.

Kocha wa Yanga, Cedrick Kaze amesisitiza kwamba mchezaji huyo ni miongoni mwa nyota ambao watafanya vizuri zaidi kwenye mzunguko wa pili na kurahisisha njia ya ubingwa wa Yanga msimu huu. Soma zaidi alichosema Kaze pamoja na mahojiano yake maalum na Mwanaspoti kwenye ukurasa wa 12&13 wa gazeti hili .