Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FIBA yatoa mipira 10 ya 3x3

FIBA Pict
FIBA Pict

Muktasari:

  • Kamishna wa ufundi wa makocha wa shirikisho la mchezo wa kikapu nchini (TBF), Robert Manyerere alisema baada ya kupokea mipira hiyo waligawa kwa wasimamizi wa mchezo huo, katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Mbeya, Arusha, Dar es Salaam na Unguja.

SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu la Kimataifa (FIBA), limetoa mipira 10 kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo wa 3x3 unaohusisha wachezaji wanne, huku wa tatu wakiwa wanacheza ndani ya uwanja na mmoja wa akiba.

Kamishna wa ufundi wa makocha wa shirikisho la mchezo wa kikapu nchini (TBF), Robert Manyerere alisema baada ya kupokea mipira hiyo waligawa kwa wasimamizi wa mchezo huo, katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Mbeya, Arusha, Dar es Salaam na Unguja.

Wakati huohuo, mashindano ya vyuo vya Tanzania ya 3x3 yatafanyika Desemba mwaka huu na yalikuwa yafanyike kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba mwaka huu, kabla ya kuahirishwa kupisha Ligi ya Kikapu la Taifa (NBL) inayoendelea mkoani Dodoma.

Alisema baada ya kufanyika mashindano hayo, wanakusudia kuandaa pia ya vyuo vikuu vya Afrika mashariki na kati.