Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fenerbahce yamvutia kasi Samatta Ulaya

Muktasari:

Kabla ya hata kujiunga na Aston Villa wakati wa dirisha la usajili la Januari, Fenerbahce ilikuwa miongoni mwa klabu ambazo zilikuwa zikiwania saini ya Samatta

Miamba ya soka ya nchini Uturuki, Fenerbahce inaifuatilia kwa karibu timu ya soka ya Aston Villa kwenye vita ya kujinasua kushuka daraja kutokana na mpango ilionao wa kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ‘Samagoal’.

Kwa mujibu wa gazeti la Takvim la Uturuki, Fenerbahce wanajiandaa kutuma ofa ya kumnasa kwa mkopo wa msimu mzima nahodha huyo wa timu ya taifa la Tanzania ‘Taifa Stars’ ikiwa timu hiyo itashuka daraja.

Gazeti hilo limepambwa na kichwa cha habari kikubwa kisemacho ‘Fenerbahçe’nin hedefinde Aston Villa’li Mbwana Samatta var’ wakiwa na maana kuwa Samatta ndiye chaguo lao.

Fenerbahce wana imani kubwa kuwa huenda wakamnasa mshambuliaji huyo kutokana na kipengele kilichopo katika mkataba wake kuwa anaweza kuondoka Villa endapo timu hiyo itashuka daraja.

Kabla ya hata kujiunga na Aston Villa wakati wa dirisha la usajili la Januari, Fenerbahce ilikuwa miongoni mwa klabu ambazo zilikuwa zikiwania saini ya Samatta kipindi hicho akiichezea KRC Genk ya Ubelgiji ambayo aliifungia mabao 56 ndani ya msimu mitano katika Ligi Kuu.

Katika vita hiyo, Fenerbahce wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wao, Galatasaray ambao nao wameonyesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba ya Ligi Kuu Bara na TP Mazembe ya DR Congo.

Wakati hesabu za Fenerbahce na Galatasaray zikiwa ni kumsajili Samatta kwa mkopo kama klabu yake itashuka daraja mambo ni tofauti kwa Samatta ambaye anapambana kuinusuru timu hiyo isishuke.

Samatta alikuwa sehemu ya kikosi cha Aston Villa ambacho juzi Jumanne kiliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal na kusogea hadi nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 34 sawa na Watford ambao wapo nafasi ya 18.

Akizungumzia mazingira waliyonayo Aston Villa kwa sasa, baba wa nahodha huyo wa Taifa Stars, Ally Pazi alisema yanatia moyo tofauti na mwanzo.

“Ushindi dhidi ya Arsenal umewapa nguvu nadhani watafanya vizuri pia kwenye mchezo wao wa mwisho,” alisema.

Aston Villa watacheza dhidi ya West Ham kwenye mchezo wao wa mwisho huku Watford ambao wapo nafasi ya 18 wakicheza dhidi ya Arsenal, Bournemouth ambao wapo nafasi ya 19 wakiwa na pointi 31 watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Everton. Jumapili itakuwa ya moto.