Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali Yanga, Coastal kuhamishwa Arusha yasipofanyika haya...

Sheikh Amri Abeid kufumuliwa upya

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewapa siku saba wamiliki wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kukamilisha marekebisho ili mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) inayotarajiwa kuchezwa Julai 2, ipigwe

Akizungumza jijini hapa, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alisema endapo watashindwa kukamilisha marekebisho hayo watatengua. Fainali hiyo itazikutanisha Yanga na Coastal Union.

“Nimekuja Arusha kufanya ukaguzi wa miundombinu ya uwanja kama maandalizi ya mechi kubwa ya fainali ya Kombe la Shirikisho, lakini nasikitika kuwa maelekezo ya marekebisho tuliyoyaacha hayaridhishi hasa vyumba vya kubadilishia nguo,” alisema Kidao

Alisema maelekezo waliyoyatoa eneo la kuchezea yamerekebishwa kwa kiwango kizuri, lakini vyumba vya kubadilishia nguo bado hakuridhishi hivyo kutoa muda huo wahusika kukamilisha. “Tumezungumza na uongozi wa uwanja ambao ni CCM juu ya marekebisho hayo yafanyike ndani ya siku saba na tumekubaliana nao, hivyo wiki ijayo tutakuja na Kamati ya Mashindano kuukagua, endapo hawatakamilisha tutahamisha mchezo huo kwenda uwanja utakaokuwa umekidhi vigezo,” alisema.