Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dodoma Jiji yamng'oa Tunisia Waziri Jr

Dodoma Jiji yamng'oa Tunisia Waziri Jr

Muktasari:

  • Waziri Jr alikaribia kusainishwa na Dodoma Jiji kwenye dirisha kubwa lililopita, kabla ya kutimkia nje ya nchi na sasa amerudishwa.

Dodoma. SASA ni rasmi mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Waziri Junior ni mali ya Dodoma Jiji baada ya awali kuwaponyoka dakika za mwishoni.

Dodoma iliyokaribia kumnasa mshambuliaji huyo siku ya mwisho ya usajili wa dirisha kubwa, lakini ilishindikana kutokana na uwepo wa dili la kujiunga na timu ya nchini Tunisia.

Licha ya kudumu nchini Tunisia kwa miezi kadhaa, mshambuliaji huyo alikuwa bado hajasaini mkataba na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini humo, ikiwapa mwanya Dodoma Jiji kumrudisha kwa kipengele maalum.

Hii ni kusema kwamba, Dodoma Jiji imelazimika kumng'oa nyota huyo mdomoni mwa klabu ya Tunisia (jina kapuni), huku ikiweka uwezekano wa kuuzwa kwenye timu hiyo wakati wowote akihitajika.

Dodoma Jiji yamng'oa Tunisia Waziri Jr

Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Fourtunatus Johnson, ambaye alilazimika kusafiri hadi nchini Tunisia kwenda kumshawishi mshambuliaji huyo kurudi nchini, ameliambia Mwanaspoti kuwa, ilikuwa ngumu kufanikisha dili hilo, ndio sababu wameweka urahisi wa kumuachia pindi atakapotakiwa na klabu hiyo ya Tunisia.

"Tumefanikiwa kumsajili kweli Waziri Junior baada ya dirisha lililopita dili kutibuka mwishoni, imebidi tumfuate Tunisia ili kutimiza hilo, kama timu tulipomchukulia itamhitaji hatutasita kumuachia wakati wowote" alisema Johnson.

Licha ya afisa habari wa timu hiyo, Moses Mpunga kutoweka wazi lakini kuna uwezekano mkubwa, Waziri Junior akawa mrithi wa David Ulomi, aliyeuzwa nchini Sudan ambapo mshambuliaji huyo atakabidhiwa jezi namba saba iliyokuwa inavaliwa na Ulomi.